Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | Cath Lab : Mashine ya Kisasa Kabisa kwa Ajili ya Matibabu ya Moyo Yatua Muhimbili

Waandishi wa habari wakiangalia kifaa hicho - Picha @ Global Publisher

Hospitali ya Muhimbili imepata mashine ya kisasa zaidi kwa ajili ya kusaidia katika upimaji na utibabu wa matatizo ya moyo. Kifaa hicho cha teknolojia ya juu kinafahamika kwa jina la Cath Lab  na kuanzia sasa kitaanza kutumika katika hospitali hiyo. Kirefu cha neno Cath Lab ni ‘Cardiac Catheterization Laboratory’.

Waandishi wa habari wakiangalia kifaa hicho - Picha @ Global Publisher
Waandishi wa habari wakiangalia kifaa hicho – Picha @ Global Publisher

Kifaa hicho chenye thamani ya takribani shilingi bilioni 4 (Dola milioni 2 za kimarekani) kitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wingi wa wagonjwa wa moyo kutegemea kupata matibabu hayo nje ya nchi. Sifa kubwa ya kifaa hicho ni pamoja na uwezo wa kuchunguza na kutibu matatizo ya moyo bila uhitaji wa upasuaji (oparesheni). Katika ufanyaji kazi wake mgonjwa atachomwa na kuingiza kitu kidogo kwenye moja ya mshipa wake na kisha mashine hiyo itafanikiwa kufanya tathmini ya moyo na mishipa yote muhimu kuweza kutambua tatizo.
Watu wenye matatizo madogo madogo ya mishipa ya damu wataweza kupata matibabu hayo kuanzia sasa katika hospitali hiyo, kumbuka matatizo haya yasipotibiwa haraka mtu anaweza kupata mshituko wa moyo (heart attack).
Kitu kingine kizuri kuhusu kifaa hicho ni jinsi gani inachukua muda mfupi sana kumuhudumia mgonjwa mmoja, inasemekana uchunguzi mzima unaweza chukua takribani dakika 30 tuu. Katika nchi za Afrika Mashariki ni Uganda na Kenya tuu ndizo nazo zinakifaa hicho.Dr-Robert-Mvungi-muhimbili
Kwa kuwa kifaa hicho kinaitaji usimamizi na uendeshaji wa watu waliobobea kwa sasa hakuna mtanzania anayehusika katika utumiaji wa kifaa hicho. Uongozi wa kitengo husika cha matibabu ya moyo kimesema watakuwa wanategemea madaktari bingwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuendesha kifaa hicho. Kwa sasa kuna kundi la madaktari kutoka nchini Saudi Arabia ndio watakuwepo hadi tarehe 18 mwezi huu. Baada ya hapo wanategemea kutakuwa na kundi jingine la madaktari kutoka nje, nia kuu ni kwamba katika kipindi hichi madaktari wazawa watakuwa wanajifunza zaidi.

Post a Comment

0 Comments