Na Andrew Chale, Nairobi, Kenya
Wataalamu
wa kichunguzi na wanasayansi wa Mazingira, wameelezea kuwa visiwa
vilivyopo ndani ya bahari ya Hindi vinatarajiwa kutoweka duniani
kutokana na mabadiriko ya tabia nchi inayoikumba dunia kwa sasa ikiwemo
upungufu wa kimo cha bahari, ukame na hali ya joto sehemu mbalimbali
duniani.
Hayo
yameelezwa jijini hapa katika mafunzo juu ya kuripoti habari za
mazingira na mabadiriko ya tabia nchi (Climate Change) mafunzo
yaliyoanza jana Juni 1, 201a5 ambayo ni maalum kwa wandishi wa habari
wanaoandika katika mitandao ya kijamii blog na tovuti kutoka nchi
mbalimbali za Afrika, zikiwemo Tanzania, Rwanda, Madagasca, Kenya na
Ufaransa ambaoyo ni ya wiki mbili ambao pia ni mkutano wa maandalizi
kuelekea katika kongamano la mazingira litakalofanyika jiji la Paris,
Ufaransa, Julai na Desemba mwaka huu.
Akielezea
hali hiyo, Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na
mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru,
alibainisha kuwa, visiwa vingi ndani ya bahari ya Hindi ikiwemo
Mombasa, Comoro na Madagasca vimo hatarini kutoweka kabisa duniani
kutokana na tabia nchi (Climate Change).
“Utafiti
mbalimbali umefanyika na kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Dunia
itaingia katika matatizo makubwa. Hasa kwa upande wa bahari ardhi
iliyo ndani yake kuja kumezwa ikiwemo visiwa vya Zanzibar, Madaga”
alieleza Kabukuru ambaye pia ni mchambuzi na mtafiti wa masuala ya
mazingira ya ukanda wa bahari anayefanya kazi zake nchini Kenya.
Kwa
Tanzania tayari athari mbalimbali zimeanza kujitokeza kutokana na tabia
nchi ambapo kwa sasa mmomonyomko wa radhi umeweza kukumba maeneo zaidi
ya 148 ambayo yanaingia maji ya chumvi huku wakulima wakishindwa
kuendelea na kilimo cha kawaida.
Mkutano
huo ulioanza leo Juni Mosi, umeandaliwa na Media Coperation CFI kutoka
nchini Ufaransa ulio na lengo la kutafuta njia mbadala juu ya kuripoti
habari za mabadiliko ya tabia nchi kwa ushirikiano wa Ubalozi wa
Ufaransa Kenya na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kwa
washiriki wa Tanzania,wanawakilishwa na Andrew Chale mtandao wa
modewjiblog na Dotto Kahindi mwandishi wa habari wa kujitegemea.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena