Kwa takribani wiki mbili sasa neno ‘rushwa’ limekuwa likiliandama sana shirikisho la soka duniani FIFA.
Wiki iliyopita maafisa 10 wa shirikisho hilo walikamatwa na serikali
ya Marekani kwa kujihusisha na skendo ya ubadhirifu wa £100m, jambo
ambalo lilipelekea wadau mbalimbali kumuomba Rais wa shirikisho hilo
Sepp Blatter kujiuzulu.
Hata
hivyo Blatter amegoma kufanya hivyo, lakini ikiwa suala la ubadhirifu
wa £100m likiwa bado la moto, leo hii umetolewa ushahidi kwamba katibu
mkuu wa FiFA Jerome Valcke alihusika na rushwa ya $10m kutoka kwa
shirikisho la soka la Afrika ya kusini.
Kwa mujibu wa mkuu wa shirikisho la soka la SA, Danny Jordaan,
amethibitisha kwamb ni kweli nchi hiyo ililipa kiasi hicho kwenda Raisi
wa shirikisho la soka la CONCACAF wa wakati huo, Jack Warner mnamo
mwaka 2008, kwa jili ya kusaidia maendeleo ya soka barani humo na sio
rushwa iliyosaidia nchi hiyo kupata uenyeji wa kombe la dunia mwaka
2010.
Kwa upande wa FIFA wamemtaja, muargentina Julio Grondona ndio
alikuwa mhusika mkuu ktika kuidhinisha malipo hayo ya $10 million.
Grondona alikuwa na cheo cha umakamu wa raisi na pia mwenyekiti wa
kamati ya masuala ya fedha ya shirikisho hilo, hata hivyo Grondona
alifariki dunia mwaka 2014.
Kauli ya FIFA kwamba Grondona ndio alitoa ruhusa ya kufanyika kwa
malipo hayo ya rushwa inaonekana kumsafisha Jerome Valcke, baada ya
gazeti la New York Times kutoa taarifa kwamba Valcke ndio aliyeidhinisha
malipo hayo ya rushwa.
Lakini leo hii umetolewa ushahidi wa barua unaonyesha Valcke ndio
aliyeidhinisha malipo hayo ikiwa ni rushwa kutoka nchi ya South Africa
ambayo ilipewa uenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010.
Mwendesha mashtaka wa Marekani amesema kwamba South African ililipa
fedha hizo kwa Mr. Warner – ambaye wakati huo alikuwa makamu wa raisi wa
FIFA ili kutimiza ahadi yao baada ya kupewa haki ya kuandaa kombe la
dunia 2010.
Fifa iliichagua South Africa kuandaa fainali hizo mbele ya Morocco.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena