Header Ads Widget

Responsive Advertisement

BVR TARIME-RORYA | WAMASAI WALIPATA WAKATI MGUMU KUJIANDIKISHA, FAHAMU HAPA

Waamasai wanaotembeza madawa ya miti shamba Mjini Tarime mkoani Mara wamepata wakati mgumu kuandikishwa kwa ajili ya kupata vitambulisho baada ya kudaiwa kutotambuliwa na wenyeviti wa mitaa kutokana na kutokuwa na makazi wala kutofahamika mitaa wanakoishi.

Wakiwa wamejipanga kwenye mistari kungoja kujiandikisha  kwenye kituo cha uandikishaji wa vitambulisho mtaa wa Mwangaza Kata ya Nyamisangura mjini Tarime Mwenyekiti wa Mtaa Abdalla Mauridi aliwahoji wamasai watatu kuwa  wanaishi ubarozi wa nani na kama wamepanga wamepanga kwa nani ambapo walisema hawana makazi maalumu.

vijana wa kimasai



Musa Oneremit alisema kuwa wao ni wazaliwa  wa Ngorongoro –Arusha  wako Tarime  tangu januari wakijishughulisha na biashara ya kutembeza mitaani dawa za mitishamba na kwamba  wao  uzungusha biashara na ifikapo usiku ulala kwenye gest  mbalimbali mjini humo.

“Sisi tunatembeza dawa tumekuja Tarime tangu mwezi wa kwanza tunaweza kukaa hadi miezi sita kisha tunarudi Ngorongoro kutafuta dawa tunapokuwa hapa tunatembeza madawa kwa watu usiku ukifika tunalala kwenye Gesti sisi ni watanzania tunaomba tupate vitambulisho kura tutapigia hapa Tarime”alisema Oneremit.



Lebahati Olekambusi  alisema iwapo watakosa fursa ya kuandikishwa kupewa kitambulisho ni kutowanyima haki yao ya kupiga kura,Pamoja na Maelezo yao Mwenyekiti  Mauridi aliwakatalia kujiandikisha na kuwataka wamasai hao waende uongozi wa juu kwa mtendaji wa kata au kwa Mkurugenzi wa Halmashauri  wakajieleze watakavyosaidiwa kwakuwa si wakazi wa mtaa wake.

 Mwananchi ikiwa kwenye kituo hicho cha kupigia kula na kushuhudia kinachoendelea ililazimika kumtafuta kwa simu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Venus Mwamengo na kueleza kilichojili kwa watu hao ambapo Mkurugenzi huyo alifika maramoja kwenye kituo kuwasikiliza.

Mwamengo aliwahoji kama wanavitambulisho vyovyote vinavyowatambua kuwa ni Raia wa Tanzania ambapo Musa Onekemit alitoa kitambulisho cha uanachama cha CCM huku wngine wakiwa hawana kitambulisho chochote,walikataliwa na hivyo kutakiwa kujaza fomu kwenda kwa Mkurugnzi ili wachunguzwe zaidi .

“Kuna wamasai wa Tanzania na wa Kenya ili tuthibitishe kuwa ni wazaliwa wa Ngorongoro ingieni kwa waandikishaji wa bvr mjaze fomu  mzilete kwa Mkurugenzi sisi tunataraibu zetu tutafatilia huko ngorongoro kujua kama ni wazaliwa  kisha mtapewa vitambulisho hata kama muda wa uandikishaji ukipita tukiwathibitisha nina kibari cha kuwapeni Vitamburisho”alisema Mwamengo.

Majibu hayo  yaliwapa matumaini na kisha kujaza fomu ambazo zitashughulikiwa ndani ya siku mbili na baada ya kuthibitika kuwa ni wazaliwa wa Ngorongoro watajiandikisha na kupatiwa vitambulisho,na muda si punde wamasai wengine watano walijitokeza kwenye kituo hicho na kujaza fomu baada ya kupatiwa maelekezo


Post a Comment

0 Comments