Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu
ya Chama Cha Mapinduzi (CC) imeagiza kurudiwa kwa uchaguzi katika
majimbo matano yaliyopo Tanzania Bara kutokana na dosari mbalimbali
zilizojitokeza katika mchakato wa kura ya maoni.
Majimbo yanayotakiwa kurudia uchaguzi wa kura ya maoni ni pamoja na Makete, Busega, Ukonga, Rufiji na jimbo la Kilolo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema mchakato huo utarudiwa siku ya
Alhamisi Agosti 13 mwaka huu.
Amesema baada ya uchaguzi huo matokeo yatapelekwa katika vikao vinavyoendelea kwa ajili ya uamuzi.
Akizungumzia kuhusu vikao vinavyoendelea katika ukumbi wa NEC mjini
Dodoma amesema vikao hivyo vinaendelea vizuri ambapo jana kikao cha
kamati ya maadili kiliendelea mpaka usiku.
Amesema leo wanatarajia kumaliza kikao cha Kamati Kuu ambapo kesho na
kesho kutwa watamaliza na kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho (NEC)
kama ilivyopangwa
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena