Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akifafanua uchafuzi unaofanywa na baadhi ya wanunuzi na wakulima kwa kuchang’anya pamba, maji, mchanga na mbegu kwa lengo la kuongeza uzito. |
MAWAKALA wa
ununuzi wa Pamba wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamelalamikiwa
kuhusika katika kuharibu ubora wa zao hilo kwa kuchanganya mchanga na
mawe wakati wa ununuzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake mwenyekiti wa umoja
wa wanunuzi wa Pamba kanda ya ziwa (UMWAPA) Mhoja Nkwabi amesema hali
hiyo imepelekea Pamba kushuka thamani katika soko la Pamba duniani.
Ukiitizama kwa harakaharaka pamba hii unaweza kuiona kuwa iko salama, ila ukichukuwa jukumu la kuigusa ndipo utagunduwa kuwa kunachembe chembe za mchanga na uchafu mwingine ndani yake. |
Nkwabi amesema kuwa Mawakala wa ununuzi wamekuwa wakihujumu makampuni
ya ununuzi wa Pamba kwa kuweka vitu vinavyoongeza uzito kwa manufaa yao
hali ambayo ni kuyaibia makampuni hayo pamoja na wakulima huku serikali
ikishindwa kutatua tatizo.
Ameongeza kuwa wakulima wamekuwa wakilalamika kuhusiana na kushuka
kwa bei ya zao hilo na hii inatokana na makampuni yanayonunua Pamba
kulazimika kufanya hivyo kutokana na Pamba kushuka ubora katika soko
lake.
Katika hatua nyingine amesema Mei 3 mwaka huu umoja huo ulishakutana
na serikali katika kutafuta suluhu ya tatizo hilo na kuiomba iwe inateua
mawakala na itengeneze mfumo wa kuwabana pindi wanapobainika kufanya
hivyo.
Hata hivyo amewaomba wakulima na serikali kutoa ushirikiano katika
makampuni yanayonunua Pamba nchini kuwabaini wanaotumia mfumo wa
kuongeza vitu vizito kwenye Pamba safi ili wapate kilo nyingi.
Kumekuwa na matatizo ya wakulima kulalamikia makampuni ya ununuzi na
serikali kwa ujumla kushusha bei ya zao hilo kila msimu wa ununuzi
unapofika bila hatua zozote za ufumbuzi kufanyika.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena