Rais John Magufuli leo amekutana na balozi wa Israel Yahen Vilan ikulu na kuzungumzia mikakati ya Tanzania kutaka kuwa na ukaribu zaidi na nchi hiyo.
Katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa
imesema moja ya mambo muhimu ni pamoja na Tanzania kuanzisha ubalozi
wake nchini Israel hivi karibuni pamoja na kujenga mahusiano mazuri
baina ya nchi hizo.
Pia balozi huyo ameahidi kufikisha ujumbe wa Rais Magufuli kwa Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyau na kuanzisha ofisi ya kutoa huduma ya visa hapa nchini.
Taarifa hiyo ilisomeka hivi…
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena