Serikali
kuendelea kutoa elimu ya Uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali
kwa wananchi ili waweze kunufaika na rasilimali zote zilizopo katika
maeneo yao kote nchini.
Kauli hiyo
imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya
Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Bw.Carlos Mbuta
wakati wa mkutano na vyombo vya Habari ikiwa ni moja ya mikakati ya
Serikali katika kuelimisha umma kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali
ikiwemo ardhi.
Akifafanua
Mbuta amesema kuwa Elimu hiyo itawasaidia wananchi kungamua na kufanya
maamuzi sahihi pale wanapotaka kutumia rasilimali zilizopo katika
kujiletea maendeleo.
’Elimu ya
mazingira imejumuishwa katika mitaala ya shule zetu hapa nchini ili
kujenga uelewa kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali alisisitiza Mbuta
Akizungumzia
faida za Elimu ya Mazingira kutlowa mashuleni mbuta alibainisha kuwa
itasaidia kujenga kizazi chenye uelewa na uwezo wa kutumia rasilimali
zilizopo kwa kuzingatia sheria na kanuni.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. George Pangawe alitoa wito kwa
wananchi kufuata taratibu zote za kisheria pale wanapotaka kuendeleza
Kipande chochote cha ardhi.
Aliongeza kuwa
Serikali kupitia Wizara yake inasimamia matumizi sahihi ya uendelezaji
wa ardhi na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika
kusimamia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta ya ardhi.
Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Baraza la Taifa
la Mazingira pamoja na Halmashuri zote nchini zimekuwa zikisisitiza
kuhusu elimu ya uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali ili ziweze
kuwanufaisha wananchi.
wa Habari (Hawapo Pichani)
kuhusu wananchi kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji nchini pale
wanapotaka kuendeleza ardhi kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya
Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta na kulia ni
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni
Bi. Juliana Letara.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu
ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta
akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu elimu ya
uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali ili waweze kunufaika na
rasilimali hizi ambapo elimu hiyo imeingizwa katika mitaala ya elimu
hapa nchini kulia ni Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya
Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George Pangawe.
Mkuu wa Idara ya Mipango
Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara
akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kulia
ni Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na
Maendeleo ya Makazi George Pangawe na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha
Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena