July 16 2016 ilikuwa ni zamu ya wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wao wa tatu waKundi A wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu ya Medeama SC ya Ghana.
Kabla hata ya mchezo wa leo July 16 Yanga walikuwa nafasi ya mwisho kutokana na kukubali vipigo viwili mfululizo vya michezo yao miwili ya mwanzo, mchezo wa kwanzaYanga walicheza Algeria na MO Bejaia na kukubali kipigo cha goli 1-0 na baadae kipigo cha goli 1-0 kutoka TP Mazembe ya Congo uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mchezo wa July 16 Yanga wanaofundishwa na kocha wao muholanzi Hans van der Pluijm, walikuwa wanahitaji ushindi wa aina yoyote ili waweze kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuwania kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, hata hivyo Yangawamelazimishwa sare ya goli 1-1.
Kikosi cha Yanga ambacho kilionekana kuwa na morali ya kuondoka na point tatu na kusahaulisha mashabiki wake vipigo viwili vya mwanzo, walianza kupata goli dakika ya 2 kupitia kwa Donald Ngoma ambaye alitumia vyema pasi ya mzimbabwe mwenzakeThabani Kamusoko, furaha ya Yanga ilizimwa dakika ya 17 baada ya Benard Dansokuisawazishia Medeama goli na kuifanya Yanga endelea kuwa nafasi ya mwisho katika msimamo wa Kundi A.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena