Header Ads Widget

Responsive Advertisement

JIFUNZE ~ Unamfaham JOHN STEPHEN AKHWARI? Mtanzania Alieacha Historia Inayoishi Milele kule Mexico

Image result for John Stephen AkhwariIlikuwa ni siku ya jumapili mchana mwaka 1968 mwezi wa kumi wakati wa baridi kali, kundi la wakereketwa wa mchezo wa riadha waliokuwa wakitazama michuano ya Olimpiki ndani ya uwanja wa Mexico city, idadi kubwa ya watu iliweza kushuhudia ushindani mkali uliokuwa ukiendelea kati ya washiriki 74 ndani ya uwanja huo, na moja kwa moja kabla ya lisaa limoja kupita katika mbio hizo za kilomita 42, Mamo Wolde wa taifa la Ethiopia aliweza kuingia uwanjani hapo na kumaliza mbio zake mbele ya wakimbiaji wenzake waliokuwa wakimfatia nyuma na kuibuka kuwa mshindi miongoni mwa washiriki wote waliokuwa wakishiriki mbio hizo.Ikiwa ni muda wa jioni sana na kiza kimeanza kutanda hata mashabiki wengi wa mchezo huo wakianza kutoka uwanjani hapo na kubaki idadi ndogo ya watu, ghafla watu walishtushwa na mlio wa pikipiki yenye king’ora cha polisi iliyokuwa ikimsindikiza mkimbiaji mmojawapo aliyekuwa akiingia uwanjani hapo huku akiwa ameumia sana na kufungwa bandeji huku akivuja damu katika mguu wake mmoja; huyu si mwingine alikuwa ni John Stephen Akhwari kutoka nchini Tanzania. Akhwari alipata majeraha makubwa baada ya kukimbia kilomita kama 30 akateleza na kudondoka katika  barafu iliyokuwa imetanda katika barabara za Mexico na hapo ikampelekea kuumia vibaya katika mguu, ndipo madaktari wakamtibu na kumshauri hasiendelee na mbio lakini aliamua kuendelea ili kumalizia kilomita 12 zilizobaki.Alipofanikiwa kuingia uwanjani na kufikia mstari wa mwisho wa kumaliza mbio zake, waandishi wa habari na watu waliokuwa karibu nae waliweza kumuuliza swali, ni kwa nini hakuamua kuacha kukimbia kwa kuwa alikuwa ameumia sana na tayari hakuwa na nafasi yoyote ile ya kushinda medali? Akhwari aliwajibu kwa kusema, “Nchi yangu (Tanzania), haijanituma kuja kuanza mbio ila imenituma kuja kumaliza mbio.” Jibu hili ndio lililomfanya Akhwari kutambulika kama shujaa katika mchezo wa riadha ulimwenguni hadi hivi leo. Akhwari aliweza kuonyesha moyo wa ushujaa na kutokukata tamaa mapema katika mbio zake na hii ilikuwa sababu ya kumfanya kuwa miongoni mwa watu mashujaa hadi hivi leo pamoja na kutokupata ushindi na medali yoyote, bali maneno yake ya kishujaa yanamfanya kukumbukwa kwenye mchezo huo hadi hivi leo.“Even if you fall on your face, you’re still moving forward.”-Victor KiamHivi ndivyo inavyotakiwa kwa mtu yoyote aliye na safari ya kuelekea katika kutimiza ndoto zake, weka akilini kwamba unahitaji kuweka lengo la kumaliza kile kitu ulichoanza kufanya pasipo kuishia kati. Umeumbwa kwa ajili ya kusudi maalum hapa duniani. Ni vizuri ufanye maamuzi na kupanga vyema huku ukitia mkazo na bidii ya kufanikisha jambo lolote ulilolianza. Akhwari anatuonyesha ni jinsi gani yeye binafsi alivyokuwa akitazamisha macho yake yote kwenye picha ya kitu kilicho mpeleka nchini Mexico, kuliko kutazamia maumivu aliyokuwanayo na hali iliyokuwa ikitaka kumzuia kutimiza ndoto yake ya kumaliza mbio.Kuna mambo 3 ambayo tunajifunza kutoka katika habari hii ya Akhawari:1: Amua kumaliza ulichokianza.Watu wengi sana wameshindwa kufanikiwa kwa sababu ya tabia ya kutokumaliza mambo yao wanayoanza kufanya; watu hawa ni wenye kushika kila kitu na kila wanalogusa hawamalizi na badala yake wanashika hiki na badae wanahamia kwenye kingine. Angalia ni jambo gani ulilokuwa umeanza kufanya lakini leo hii umekata tamaa na ukaacha kulifanya hadi mwisho ili kuleta matokeo makubwa katika maisha yako. Jiulize ni malengo mangapi uliyokuwa ukihitaji kuyafanikisha ndani ya mwaka huu na hadi hivi sasa umeweza kuyafanikisha sawa na ulivyokuwa unataka.Mojawapo ya tabia inayomtofautisha mtu aliyefanikiwa na ambaye hajafanikiwa ni kwamba, watu wengi waliofanikiwa huwa ni watu wenye kushikamana na jambo moja hadi mwisho kabla ya kuamia jambo lingine, ila kwa upande wa watu wasiofanikiwa hii ni tofauti kwao, kwani wengi wao ni watu wa kujaribu kufanya kila kitu wanachoona kinafaa kwao na hii imekuwa sababu kubwa kwao ya kutokufanikiwa katika maeneo mengi ya maisha yao. Kama unahitaji kufanikiwa na kutimiza ndoto zako ulizonazo ni vizuri utambue unahitaji kumaliza kila jambo unalolianza pasipo kuishia kati, hata kama kutatokea vikwazo mbele yako unapaswa kusimama imara kwa ajili kuhakikisha unashinda na kufanikisha ndoto yako uliyonayo.2: Usiangalie mazingira magumu uliyonayo bali kaza mwendo kumaliza mbio zako.Akhwari pamoja na kupata ajari na majeraha makali baada ya kuanguka na kuumia mguu katikati ya mbio zake, lakini hakuruhusu nafasi ya kuacha kukimbia na badala yake alitumia mazingira yale ya kuumia kama changamoto kwake inayotaka kumzuia hasimalize mbio zake. Kwake binafsi suala lilikuwa si kuacha mbio bali kukimbia na kumaliza mbio zake alizozianza hata kama hatokuwa mshindi wa mbio hizo ila amefanikiwa kutimiza mwisho wa mbio zake zilizomfanya awepo mjini Mexico.Angalia ni mara ngapi umekata tamaa hata kuacha kutimiza malengo mazuri na makubwa uliyokuwa nayo kwa sababu ya hali ngumu iliyojitokeza mbele yako kwa ajili ya kukuzuia kusonga mbele. Jiulize ni kwa nini umekwama hadi muda huu kwenye jambo ulilokuwa ukitazamia kulifanikisha katika maisha yako? Ni nini kilichokufanya ukwame katika kufanikisha malengo na ndoto yako uliyonayo? Mara nyingi si watu wengi walio na tabia ya kufanya tathmini na kujiuliza maswali ni jambo gani lililowafanya kukwama na kutokuendelea mbele katika safari ya kutimiza ndoto zao. Amua kuangalia kwa umakini kuanzia sasa na kufatilia ni kikwazo gani kilichokufanya kukata tamaa hata kushindwa kutimiza ndoto yako.“It’s not who you are that holds you back, it’s who you think you’re not.”-John Assaraf3: Weka umakini kwenye picha unayoiona mbele yako.Kama unahitaji kushinda na kufanikisha malengo yako mengi uliyonayo ni muhimu sana kwa kupitia akili yako kujenga tabia ya umakini kwenye eneo moja unalotaka kuleta ushindi juu yake. Huwezi kufanikiwa nje ya picha unayoiona ndani yako, huwezi kufanikiwa nje ya mawazo uliyojenga ndani yako. Hii ni kwa sababu mawazo ya mtu ni mjumuisho mzima wa namna mtu anavyofikiri na kuona ndani yake, na kutaka kutenda kwa kuchukua hatua kwa anachokiwaza. Mawazo ndio yanayotengeneza picha ya maisha yako unayotaka hapo badae ukiwa unaishi leo, kama utawaza vizuri basi fahamu maisha yako yatakuwa sawa na ulivyowaza, na kama utawaza vibaya basi maisha yako yatakuwa kwenye hali mbaya hapo badae.Amua kuweka umakini (focus – concentration) kwenye picha unayoiona ndani yako kuhusu unachokitaka kitokee kwenye maisha yako kuliko hali halisi ya nje inayotaka kukukatisha tamaa ya kufanikisha malengo yako. Jiulize ni picha gani uliyonayo au unayoiona hadi sasa kuhusu maisha yako ya badae? Kumbuka picha hiyo ndio maisha yako halisi ya badae, huwezi kufanikiwa nje ya picha unayoiona ndani yako.JIAMINI NA AMINI UNAWEZA. ISHI NDOTO YAKO.

Post a Comment

0 Comments