Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Rorya | Bodaboda wilayani Rorya wapatiwa mafunzo ya usalama barabarani

Image may contain: one or more people, people sitting and indoor
Mbunge wa Rorya mh Lameki AIRO pamoja na mkuu wa shule ya mafunzo ya udereva TARIME COMMUNITY DRAIVING SCHOOL (TCDS)Ndg Ernest A Oyoo baada ya kukaa na kujadiliana namna ya kusaidia bodaboda wengi ambao kwa kiwango kikubwa siku za nyuma hawakuwa na ajira nawengine kuwa natabia ambazo sio nzuri hasa wengine kujihusisha na vitendo vya uhalifu waliona nijambo jema kuchukua nafasi ya kuwasaidia KWA kutoa mafunzo kwa kila tarafa ili kila boda boda aweze kuwa na leseni na kufanya shuguli zao bila kusumbuana na polisi wa usalama barabarani kwani imekuwa kero kwa polisi wa usalama barabarani wawapo kazini boda boda huona kama wana nyanyaswa kwa kutokuwa na leseni bila kutambua kwamba nikosa kuendesha chombo cha moto bila leseni.

Image may contain: 1 person
Akiongea na wanafunzi /boda boda katibu wa mbunge ISSACK MAJWALA amewatakakutumia mafunzo haya kwa umakini kwanza kutambua sharia za barabarani na kwamba kuna umuhimu wa kusomea udereva ndiyo maana kusoma serikali inamtaka kila dereva wa chombo cha moto kusoma mafunzo hayo kwahiyo kwa yeyote ambae hatatumia fursa hizi atajilaumu kwa uzembe pale atakapo kamatwa kwamba hana leseni nawakati huo aliona haina umuhimu nakuanza kusumbua diwani pale wanapokamatwa na vyombo vya usalama .mh wembe diwani wa kata ya bukwe amempongeza mbg na mkuu wa shule ya udereva tarime community driving school kwa kukubali kusaidia kutoa mafunzo haya kwani kuna watu walipata mafunzo haya mpaka Leo hawajapata vyeti vya mafunzo na kwasababu wale watu walikuja wakakusanya pesa kwa vijana na kutokomea kusiko julikana . kwakuwa gharama ya mafunzo haya Inge gharimu sh 60000/= lakinikwa sasa garama ni sh 27500/= baada ya kuchangiwa na mh mbunge amewataka wanafunzi wa mafunzo Haya kuwa makini kwa yote walio fundishwa.
Image may contain: one or more people, motorcycle, outdoor and nature
Diwani wa kata ya mirare mh nyawambo amempongeza mh mbunge kwa jambo hili LA kuondoa kero ya boda boda kutokuwa na mafunzo ya usalama barabarani nakwamba sasa lawama zitawaangukia wale wote ambao wamepuuzia mafunzo haya ambayo boda boda alitakiwa kuchangia sh 11500/= tu unapata elimu ya usalama barabarani na leseni ukiwa nyumbani .

Image may contain: 1 person, sitting and standing
Akifungua mafunzo haya kwaniaba ya OCD wa wilaya ya rorya COPLO PETER wa usalama barabarani amewataka boda boda wore wazingatie mafunzo walio yapata kwa ajili ya kutambua sharia za barabarani na alama za barabarani na matumizi yake kwani wakishikawalio fundishq na kukata leseni usumbufu wanao ona kwamba wanaupata wawapo barabarani utapungua kwa kiasi kikubwa
Mafunzo haya yaliwez kujumuisha wanawake watatu kati ya wanaume 143 nao walisema wanaomba waume wao wawe wanawaruhusu kupata mafunzo kama haya kwani kwasasa hatawao uwezo wa kujifunza na kuendesha vyombo vya moto wanao
Mkufunzi ndg Oyoo amesema kila boda boda wanapaswa kuwashukuru mh mbunge na mkuu wa chuo ambae ni yeye mwenyewe kwa kukubali kuwasaidia boda boda kwa kugarimia mafunzo haya kwani mh mbuge amechangia kila boda boda atakaeshiriki mafunzo haya kwa wilaya ya rorya sh 10,000/= nae mkufunzi kuchangia sh 7000/= na kila boda boda kuchangia sh 11500/= .
Mafunzo haya yameanzia tarafa ya girango kata za bukwe,koryo na mirare picha na kituo cha habari utegi rorya

Post a Comment

0 Comments