Mkuu wa wilaya ya Rorya Saimoni Kemori Chacha amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari kubwa kwa wale wenye mifugo kuuza mifugo nakununulia chakula.
Akizungumza na Kituo cha Habari na Mawasiliano Utegi Rorya Ofisini kwake alisema kwa sasa hali ya hewa inatisha kwa ukame na mazao yote yalio kuwa yanategemewa kukauka kwa kukosa mvua. Ameagiza wananchi kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi kama vile mtama viazi na mihogo ili kukabiliana na baa hili la njaa. Pia amepiga marufuku kutumia chakula kidogo kilichopo kwa kupikia pombe za kienyeji nakusema atakae kamatwa sheria itachikua mkondo wake. Amesema alipopita katika tarafa za suba,luo Imbo,girango na nyancha amekuta mashamba yote yamekauka kabla ya kukomaa nakuwa hali hii inatishia uhai wa wana Rorya kwa chakula. Picha na Kituo cha Habari na Mawasiliano Utegi Rorya
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena