Mkuu wa Mkoa wa Mara Dr Charles Mlingwa ametembelea zaidi ya
kaya 30 ambazo zinanufaika na mradi wa TASAF kuwasikiliza walengwa na
kuona changamoto na mafanikiyo waliyo yapata kutokana na mradi.
Akiwa
kijijini Utegi amemtembelea ndgu Okeyo Ogola na kumkuta pesa anazopata
ameanza kuchimba shimo la choo na bafu na ambapo mkuu wa wilaya Saimoni
Kimori Chacha alimsaidia sementi 5 na kaimu mkurugenzi wa Rorya ndugu
Mhando kumchangia mabati matano5.ili akamilishe ujenzi wa choo na bafu.
NYANDUGA:
Ndugu Joseph Matara wa kijiji cha Nyanduga ameondolewa kwenye mpango wa
TASAF baada ya kuonekana uwezo wa kufanya kazi anao na fursa za
kiuchumi anazo ikiwepo miti ya natunda kama vile maparachichi,maembe na
shamba lenye rutuba.lakini hata pesa anazo pokea hakuonyeaha mpango hata
wakununua walau kuku.ili kuweza kusimama baada ya mradi kumalizika.
RIAGORO:
Samweli Atoo Matinde ambae ni mlemavu ni fundi baiskeli ameweza
kunufaika na mradi baada ya pesa anazopata ameweza kununua mbuzi ,kuku
na kununua mabati na kufanikiwa kujenga nyumba ya vyumba vitatu kwa kuwa
na mpango wa kujikwamua kutoka katika hali ya nyuma aliyokuwa nayo.
ambapo kwa kuonyesha jitihada hizo Mkuu wa mkoa Dr Charles mlingwa
amempa mifuko 5 ya sementi kwa ajili ya kukamilishia choo na bafu.ndugu
Samweli amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kumuwezesha atamalizia choo na bafu
lake.
INGRIJU:
Simion Choda ambae ni kipofu alipo tembelewa na
timu iliyo ongozana na mkuu wa mkoa walimpongeza kwa kutumia vizuri pesa
kidogo anayo pata ikiwa ni kusomeshea wajukuu zake na kufanikiwa
kujenga choo na bafu.ambapo mkuu wa mkoa Dr Charles alimpatia mifuko 5
ya sementi kwa ajili ya kumalizia choo na bafu.
Kwa kuhitimisha
ziara yake wilayani Rorya mkuu wa mkoa kwa Mara Dr Charles mlingwa
amesema nilazima viongozi wachukue hatua za maksudi kuhakikisha kila
kaya ina choo na bafu cha kisasa ili kupungiza magonjwa ya
mlipuko.amesema kinacho leta kipindu pindu ni kinyesi kama watu wanakosa
vyoo ma kujisaidia vichakani na inaponyesha mvua maambukizi yanakuwa
yanaenea kwa njia ya maji machafu .
Alipokuwa njiani kurudi Musoma
mkuu wa mkoa alikuta mkutano wa hadhara ulioitishwa na mh Nyawambo
diwani wa kata ya Mirare kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuchangia
ukenzi wa madarasa ya shule ya sekondari ya mirare baada ya kuepo na
upungifu wa madarasa na kusababisha wanafunzi walio chaguli mwaka Jana
kukosa vyumba vya kusomea ,ambapo mkuu wakoa Dr mlingwa aliguswa na
kuchangia mifuko 25 ya sementi kuwaunga mkono wanainchi wa mirare kwa
juhudi ya kuunga tamko la Mh. Dr John Pombe Magufuli kwa elimu bure kwa kila mtoto
anaezaliwa Tanzania.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena