Akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Mara, mkuu wa wilaya ya RORYA Mhe. Saimoni kemori Chacha amepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano na Mh Mbunge Lameck Airo kwa jitihada za makusudi za kuwaletea wananchi maendeleo.hasa kwa kipindi hiki ambacho huduma hii ya ghari inahitajika kwa ajili ya kuwasaidia kinamama wajawazito pindi wanapohitaji kupelekwa Hosp za rufaa.akiongea na wananchi kabla ya kukabidhi gari hili mkuu wa mkoa wa Mara Dr Charles mlingwa amewataka wananchi kulitunza gari hili ili lisaidie wananchi kwani litakuwa suluhisho kwa changamoto zilizokuwa zinawakabili wakina mama na watoto.
Mkuu wa mkoa amempongeza mh mbunge mh Lameck Airo kwa moyo alio nao wakuwaletea wananchi maendeleo, hasa kwa kuamua kujenga ward za mama na watoto. pia kwa kujenga na kununua majokofu ya kutunzia miili ya watu walio tangulia mbale za haki.amesema mh Lameck Airo ni mfano wa kuigwa kwani ni wabunge wachache wenye moyo kama wake kwani amekuwa kipaumbele kuchangia shughuli za kimaendeleo zinazogusa jamii.
Amesema hizo ni sera za chama cha mapinduzi na kuwataka wananchi na wapenzi wa vya vingine vya siasa wakubaliane na chama kilichopo madarakani kwani kwa sasa ndicho kimeshika hatamu.na kwamba kitakapo shinda uchaguzi chama kingine wote watakiheshimu hicho chama.lakini kwa sasa tunatekeleza sera za ccm chama chamapnduzi
Akiweka msisitizo na mkazo kuhusu wananchi kujenga vyoo na bafu amesema ni aibu kama gonjwa la kipindupindu litashindikama kuisha kisa uchafu hata sita kuwachukulia hatua viongozi wa kila eneo kwa kushindwa kusimamia zoezi LA usafi.
Nae mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya RORYA Mh. Machiwa amepongeza juhudi za serikali na mh mbunge kwa kutoa gari hili litasaidia sana kwani vituo hivi kukosa magari haya ya wagonjwa imechangia Vifo vingi pale akina mama wanapotakiwa kwenda Hosp kubwa kukosa usafiri na hata wengine kufa kwa kukosa huduma za gari la wagonjwa.
Nae mkurugenzi wa halimashauri ya RORYA ndugu Charles ameahidi kutoa sh milioni kumi 10,000,000/=kwa ajili ya kujenga chumba cha upasuaji baada ya risala kuonyesha mapungufu,kama vile chumba cha upasuaji,nyumba za wafanyakazi,panoja na kuwa na upungufu wa wafanyakazi. nae mkuu wa mkoa amekubali kuchangia mabati kwenye ujezi huo utakapo kamilika .
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Mh diwani Peter Sarungi amepongeza juhudi za serikali kwa kuboresha sekta za afya, ana imani ya kwamba hili gari likitunzwa vizuri litasaidia wananchi waishio mbali na kituo. Pia akatoa angalizo kwamba gari hili ni kwa ajili ya wanawake wajawazito na wagonjwa mahututi sio mtu hata akiugua kichwa atataka gari.
Nae mganga mfawidhi wa kituo cha afya Utegi Dr Manonga ameishukuru serikali na Mh mbunge kwa jitihada zao zilizo pelekea kupatikana kwa gari hili nakusema gari hili litasaidia sana hasa kwa akina mama,wazee,na watoto kwa ajili ya kupata huduma kwenye Hosp kubwa zaidi inapobidi.
PICHA NA KITUO CHA HABARI NA MAWASILIANO UTEGI RORYA | THOMAS NKAINA
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena