MVUA kubwa zilizoambatana na upepo mkali zimeleta maafa makubwa katika shule ya SEKONDARI KISUMWA. Mvua kubwa na upepo mkali ulio chukua takribani saa moja na robo imeleta madhara makubwa Nyumba 2 za maabara zimeanguka /zimebomoka na kuanguka chini, jengo moja la maabara limeezuliwa,madarasa matatu yameezuliwa, Vyoo vya wanafunzi na waalimu vimebomoka.
Akizungumza na kituo cha habari Ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Rorya Mhe. Saimoni Kimori Chacha amesema uharibifu ulio tokea ni mkubwa sana na amesema mkurugenzi wa halimashauri wamechukua hatua za dharura kuhakikisha wanarudisha haraka miundombinu ili wanafunzi waendelee na masomo.
Mkuu wa wilaya amewataka viongozi wanaosimamia ujenzi kusimamia kwa umakini kwani inaonyesha majengo mawili ya maabara hayakujengwa kwa kiwango cha kutosha kulingana na jinsi yalivyobomoka tofauti ya darasa ambalo liliezuliwa na ukuta kuonekana imara lakini Yale majengo ya maabara kiwango chake hakikukidhi viwango vya ubora.
Ametaka pesa za wananchi zinazoelekezwa kwenye miradi ya wananchi kuwepo na nidhamu ya usimamizi wa pesa hizo na kufanya kazi katika kiwango kinachotakiwa Picha na kituo cha habari na mawasiliano utegi Rorya
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena