Akipokea msaada huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Rorya katibu tawala Daudi Murumbe amemshukuru Mh Mbunge kwa kutekeleza ahadi yake kwa wahanga wa mvua iliyonyesha tarehe 16/3/2017 na kuezua zaidi ya nyumba 15.
Wakitembelea wahanga wa mvua hiyo, Mh Mbunge, Mkuu wa wilaya,mkurugenzi wa halimashauri,na wajumbe wa kamati ya maafa ya wilaya walishuhudia jinsi wananchi wa kijiji cha malongo INGRI CHINI walivyo pata shida ya kuezuliwa nyumba zao na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa.
Mh mbunge aliahidi kuchangia bati 100 na sementi 100 ambavyo vyote amevikabidhi Leo na kupokelewa na Daudi Murumbe katibu tawala kwa niaba ya mkuu wa wilaya. katibu tawala Murumbe amesema utaratibu wa wahanga kupokea vifaa hivyo utafanyika kwa Haraka sana ilikurudisha hali ya makazi yao katika hali nzuri.
Akiongea kwa njia ya simu mh mbunge amesema pia ahadi alizotowa za sementi 50 kila shule katika shule za Nyihara, Nyamaguku, kisumwa sekondari, bukwe, kibachiro,na baraki sisters amezikabidhi zote Leo. nakusisitiza kwamba hapa ni HAPA NI KAZI TU falsafa ya rais Magufuli.
Pcha na kituo cha habari na mawasiliano rorya
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena