Header Ads Widget

Responsive Advertisement

UTEGI | SIKU YA MAZOEZI YA KILA JUMAMOSI YA PILI YA MWEZI YAFANA UTEGI RORYA.

Image may contain: 3 people, people standing and outdoor
Katibu wa michezo wilaya ya rorya Saidi Masanja ambae ni afisa michezo wa wilaya ya rorya amepongeza maamuzi ya serikali kuweka Siku ya mazoezi kitaifa kwani mazoezi ni afya na kusema mazoezi sio kwa watu wanene tu Bali ni kwa watu wote. aliyasema hayo wakati akimkaribisha mwenyekiti wa michezo wilaya ambae ni katibu tawala wa wilaya ya rorya ndg Daudi Murumbe.
Image may contain: one or more people, people standing, tree, crowd, sky, outdoor and nature
Mwenyekiti wa michezo amewataka wananchi wawe wanajitokeza kila jumamosi ya pili ya kila mwezi kufanya mazoezi. amesema mazoezi ni jambo la mhimu kwa magojwa kama malerya na mengine yanayotokana na kutokufanya mazoezi pia akasema michezo ni ajira tofauti na watu wengine wanavyo fikiri.
Nae Mh mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo amesema mazoezi ni jambo LA muhimu sana kwa maisha ya binadamu kwani zoezi hukufanya kuwa na kinga dhidi ya magonjwa ambayo yanatokana na mwili kuwa legelege. Akasisitizia jambo la mazoezi kuwa ajenda ya kudumu na kuwataka wananchi kujitokeza kila inapofika Siku ya mazoezi ili kuweka afya sawa.
Image may contain: 2 people, people standing and outdoor
Nae Ocd wa wilaya ya kipolisi ya utegi amesema jeshi la polisi wanao utaratibu wa kila Siku wa kufanya mazoezi.kwao mazoezi ni ajenda ya kudumu ,amewataka wananchi kujiwekea utaratibu wa mazoezi ya kila Siku ili kuweka afya zao salama.
Image may contain: 2 people, people standing and outdoor


Nae Mkuu wa wilaya ya rorya Saimoni Kimori Chacha amepongeza wananchi, wafanyakazi serikalini, jeshi la polisi,uhamiaji idara ya afya na watu wa kada mbambali  kwa kujitokeza kwa wingi 
Image may contain: 1 person, standing and outdoor.
Pia amempongeza mh mbunge kwa kushiriki na mkurugenzi wa halimashauri pamoja na viongozi wa ccm wa ngazi zote wakiongozwa na katibu wa ccm wilaya ya rorya. Mkuu wa wilaya amesema jambo hili ni endelevu kwani ni agizo la serikali kua na Siku ya mazoezi kitaifa ambayo ni kila Siku ya jumamosi ya pili ya kila mwezi. Amewataka wananchi wote hususani vijana ambao wengi wao wamekuwa wakiwahi vijiweni na kukaa bila ya kufanya kazi wajiwekee utaratibu wa kufanya kazi.amewataka wananchi kulima mazao yanayo komaa kwa mda mfupi kwa kutumia mvua zinazo nyesha kwa sasa.
Image may contain: 4 people, people standing and outdoor
Image may contain: 4 people, people standing and outdoor
Image may contain: 6 people, people smiling, people standing and outdoor

Picha na kituo cha habari na mawasiliano rorya.

Post a Comment

0 Comments