Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Rorya | Mbunge wa Rorya na DC Wafanya ziara kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Rorya

Image may contain: one or more people, people standing and outdoor
Mh mbunge Lameck Airo akiongozana na mkuu wa wilaya ya rorya Saimon k. Chacha,mkurugenzi Charles Chacha na kamati ya mfuko wa jimbo wametembelea shule mpya zinazo tarajiwa kufunguliwa ifikapo mwezi wa NNE mwaka huu 2017 zitakapokua zimekamilika, ambazo ni Kibachiro,nyamaguku,nyanjogu,kyang'ombe na kyamkami.shule hizo zilijengwa na wananchi wakisapotiwa na mh mbunge, halimashauri na sasa mfuko wa jimbo kuongezea nguvu juhudi za wananchi. katika ziara hiyo mh mbunge kutoka mfukoni kwake alitoa sementi 25 katika ujenzi wa shule ya nyamaguku na mkrugenzi wa rorya kumsapoti mbunge kwa kutoa sh million tano ili ifikapo mwezi wa nne shule hiyo Iwe miongoni mwa shule zitakazo funguliwa.mkuu wa wilaya alimshukuru mh mbunge kwa jinsi anavyojitolea katika shuguli za kijamii hususani elimu,afya na maji.amesema kuna kila sababu ya kumpongeza kwa jitihada anazoonyesha katika jimbo la rorya.

Katika shule ya MSINGI nyancha bakenye mh mbunge amewapongeza kwa kujenga maboma 6 ya madarasa na kuonyesha ni jinsi gani wanaipa kipaumbele elimu kwa watoto wao.akizungumzia serikali mh mbunge amesema mambo yote mh rais anayaona kwenye mitandao na kusema mh rais magufuli alipo ona juhudi zenu ametoa sh milioni 20,000000/=I'll kusaidia hatakama sio kumaliza tatizo.
Kuhusu shule inayo jengwa mpya mh mbunge amesema serikali itaendelea kusapoti juhudi za wananchi kadri itakavyo wezekana
Image may contain: one or more people, people standing, tree, outdoor and nature
Mkuu wa wilaya amesema pesa za selikali na wahisani zinapotolewa inahitajika kuwepo nidhamu ya pesa. ili kulenga kilicho kusudiwa na si kutumia vibaya madaraka mliyo nayo. aliwaasa viongozi wa nyancha bakenye kumaliza mgogoro walio nao ili kufanya sjuguli za maendeleo. Kuhusu suala la wizi ambao umezuka kwa kasi katika kata ya kisumwa mkuu wa wilaya amesema haiwezekani mwizi akatoka mbali nakuja kuiba bila kuwa na mwenyeji ,amewataka wananchi wawataje wezi hadharani ili kupunguza tatizo hilo kwani linarudisha nyuma juhudi za maendeleo. Ili wa hukuliwe hatua za kisheria.
Image may contain: outdoor and nature
Katika shule ya SEKONDARI ya kisumwa mh mbunge alijionea jinsi shule hiyo ilivyo athiriwa na upepo kwa maabara zote 3 kuezuliwa na kubomolewa kabisa kuta zote na kuanguka chini alisema pomoja na mgao wa mfuko wa jimbo anatoa sementi 100 ili kurudisha miundo mbinu ya shule hiyo haraka ili wanafunzi waendelee na masomo.pia amekubali ombi la mkuu wa shule la kusaidia vitanda wasichana waishio Hostel kwani wamekuwa wanalala chini jambo ambalo mh mbunge alisema atashugulikia haraka swala la vitanda pamoja na vifaa vya michezo.ikiwa ni pamoja na mipira na jezi za michezo kwani yeye in mwana michezo.
Katika shule ya Sekondari ya Tai mh mbunge ametoa sh million 4 kwa ajili ya kukamilisha miundo mbinu na vifaa vya maji ili wanafunzi waondokane na shida wanayopata ya maji.
Image may contain: one or more people, people standing and outdoor
Shirati Hosp
Katika ziara hiyo pia mh mbunge amekabidhi gari la wagonjwa lililotengenezwa na kampuni yake baada ghari hilo kupata ajali na kuanguka na kuharibika vibaya sana.na Hosp ya shirati kukosa uwezo wa kulitengeneza kwa garama zilizokuwa zinatakiwa kiasi cha tsh million 60.pia mh mbunge alisamehe pesa aliyo kuwa anaidai shirati Hosp na kumwambia baba askofu kwamba pesa hiyo itumike kununulia matairi ya ghari hilo. jambo ambalo baba askofu alimpongeza sana mbunge na kumtakia kila la heri kwa kuonyesha uzalendo wa kweli kwa jamii.
Image may contain: one or more people, people standing, tree, outdoor and nature
Katika shule ya SEKONDARI ya nyanduga mkurugenzi wa rorya ndugu Charles Chacha amesema wametenga na kupeleka jumla ya sh milioni 26 kwa ajili ya kukamilishia maabara tatu ili wamafunzi wa masomo ya sayansi waweze kupaform vizuri katika masomo hayo.nae mh mbunge aliahidi kwa kuwa shule ile ya nyanduga imefanya vizuri kiwilaya anaipa motisha ya chakula kwa wanafunzi wa hostel ili waendelee kufanya vizuri zaidi hata kitaifa.
Picha na kituo cha habari na mawasiliamo rorya.

Post a Comment

0 Comments