Mahakama Mkoani Arusha leo imewaachia kwa dhamana mmiliki wa Shule ya Msingi ya Lucky Vicent, Innocent Mosha na Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Logino Vicent baada ya kusome mashtaka yanayowakabili.
Viongozi hao wa kuu wa Shule ya Lucky Vicent wameachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya TZS milioni 15 kwa kila mtuhumiwa mmoja.
Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent afikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka
Mmiliki na Makamu Mkuu wa Shule walifikishwa mahakamani leo kufuatia vifo vya watu 35 ambao walikuwa wakisafiri kwa basi la shule kutoka mjini Arusha kwenda Karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema. Polisi walieleza kuwa basi lililokuwa limewabeba waafunzi na walimu hao linauwezo wa kubeba watu 30, lakini wakati wa ajali lilikuwa na watu 38.
Waliofariki katika ajali hiyo ni wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja baada ya gari hilo kupinduka katika eneo la Rotya Wilayani Karatu Jumamosi iliyopita majira ya saa tatu asubuhi.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena