Simba imeingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambao una thamani ya Sh bilioni 4.9.
Mkataba huo, utaifanya Simba ipokee kitita cha Sh milioni 888 katika mwaka wa kwanza.
Mmoja wa Wakurugenzi wa SportPesa, Abbas Tarimba amesema Simba itapewa Sh bilioni 1 na milioni 80 katika mwaka wa mwisho wa mkataba kwa kuwa kila mwaka, fedha 5% zitakuwa zinaongezeka katika mkataba.
Kama hivyo haitoshi, Simba imepewa motisha, kuwa kama itachukua ubingwa basi ina nafasi ya kuchukua Sh milioni 100 kama zawadi au pongezi kutoka SportPesa.
Pia SportPesa wameonyesha wanachotaka ni kuona Simba inafanikiwa kweli, wametenga Sh milioni 250 wakibeba Kombe la Kagame au michuano iliyo chini ya Caf.
Udhamini huo unakuwa ndiyo mkubwa zaidi kuliko mingine yoyote ambayo Simba imewahi kuingia ikidhaminiwa.
Mkataba huo unaifanya Simba kuwa timu isiyo na hasara kama ilivyo kwa msimu huu ambao imemaliza ikicheza bila ya kuwa na mdhamini mkuu.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena