Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MAKALA | Mbivu na Mbichi Kuhusu Biashara ya Mtandao ( Network Marketing)

Image result for network marketing
Hawa ni watu wajanja tu wa hapa mjini ambao wamekuwa wakileta mawazo ambayo hayana mantiki kibiashara hivyo wajinga ndio waliwao, ukweli mgumu kuumeza. Hapa tunaongelea maisha na taaluma,kuna kitu ukikijua kuhusu biashara ya namna hii inahusisha matapeli wakimataifa wakiwalenga watu wenye kutaka mafanikio ya chap chap hivyo kuwaingiza mjini kwa kiswahili cha bongo.
Watu wengi wameingia bila kujua mtandao maana yake ni nini? Mtandao kwa lugha za kigeni ni (network), biashara ya mtandao ninayoizungumzia hapa ambao unatakiwa kujua siri yake na utata wake ni Network Marketing. Huu mfumo ulikuwa na kutengeneza msululu wa watu ambao unaweza ukawauzia bidhaa kiurahisi ni mfumo ambao unatumika na Aloe Vera, na makampuni mengine kama hayo. Kitu ambacho unajikuta unanunua kitu kwa bei kubwa huku ukiahidiwa muonekano ambaohujapata kuona. Hizo biashara ndio namna zinavyouza bidhaa zake, lakini kuna hawa wengine hawana wanachouza na wanakuahidi kupata mafanikio kwa akili za kawaida haileti maana na haitoleta maana. Ndio maana ya mtandao kwamba bidhaa imfikie mtumiaji kwa kupitia mtu fulani, na hicho ndicho kinachosababisha bidhaa kuwa ghali kuliko zingine chenye ubora huo huo.
Ni Biashara zilizopigwa marufuku nchi zilizoendelea 
Ukifuatilia mfumo wa utendaji wa hizi biashara ni lazima uwe umejisajili na kwa gharama fulani, huku ukiahidiwa kufanya kitu fulani ili uingize kiasi fulani cha pesa kwa wiki. Na baaada ya mwaka mmoja wanasema utakuwa tajiri au mtu uliyefanikiwa. Kila mtu anataka kufanikiwa, hiyo sio shida sida ni kwamba kiingilio chake ni kikubwa ambacho ndio mtaji wa mtu kuanzisha biashara nyingine na ikaweza kufanikiwa. Ukifuatilia nchi kama Brazil na marekani utagundua kuwa watu wengi wametapeliwa na mfumo wa biashara ya mtandao na wamiliki wake kufungwa jela. Kwanini wamefungwa jela, kwasababu mfumo mzima ni utapeli ka DESI , hivyo unakuja na sura tofauti tofauti.
Huwa hawana ofisi maalumu 
Wanakuja na ushawishi mkubwa ya kwamba ukiingia kwenye mtandao huo kupitia mtu fulani ndipo na wewe utaanza kupata faida kwa mtu mwingine utakaye msajili kupitia una lako. Ukiuliza ofisi zao ziko wapi wanasema kila kitu utapata kwenye mtandao fuata tu maelekezo. Kitu ambacho unatakiwa kukumbuka ni kwamba hakuna mtu ambaye utampa hela yako na akakupa zaidi ya kile ulichotoa isipokuwa kuna biashara fulana anayofanya inayojulikana kama watu wa Hisa, makampuni ya uzalishaji na kutoa huduma nk.
Kupata hela kwa watu wachache haimaanishi ni ukweli.(Pyramid scheme)
Kuna watu wanapata hela kutokana na mfumo huo, hiyo ipo (wajinga ndio waliwao) ishu ni kwamba mfumo huo huwa unafika mahali hela zinakuwa hakuna. Hela zinakuwa hakuna kwa sababu watu wakiacha kujiunga wale wote waliojiunga mwishoni hawapati kitu. hicho ndicho kilichotokea kwa DESI. Sasa hizi zinakuja staili tofauti tofauti, sasa hata watu walioenda shule wameshikwa na kamtandao fulani ka kutuma matangazo kwenye website fulani fulani. Sisi ambao tunajua ili uweke tangazo kwenye tovuti yangu kwa mfano lazima niwe nimekusajili na uwe na kibali cha kuweka tangazo hilo. Au uwe unashilikiana na makapuni ya utangazaji matangazo kama google, Yahoo, facebook nk.
Achana na ujinga fanya vitu makini.Ukiona mtu anakushawishi sana kuingia kwenye mtandao, kimbia haijalishi huyo mtu una mheshimu kiasi gani hana utofauti na tapeli. Usipende pesa za fasta fasta, wanachotaka ni hela yako na si kwamba wanataka wewe ufanikiwe. Wanachofanya wanakupa ahadi ya ndoto ambazo huwezi kukimbia ila wewe usipeleke hela yako kwa kitu kisicholeta mantiki watakufilisi na kukusababishia matatizo. Kimbia utapeli wa Mtandao, fanya Biashara halisi.

Post a Comment

0 Comments