Picha zimesambazwa mitandaoni zikimuonyesha mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu akidaiwa kuwa amelewa chakari.
Busungu anaonekana akiwa katika usingizi mkali huku pembeni yake kukiwa na chupa.
Moja
ya kundi linaloundwa na mashabiki wa Yanga la “Naipenda Yanga”,
limetupia picha hizo mtandaoni likibainisha Busungu yuko chakari mchana
huu katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam.
Juhudi za kumpata Busungu ambaye amekuwa nje ya kikosi hizo zimekuwa ngumu kutokana na simu yake kuendelea kuita.
Awali
ilielezwa, Busungu aliondolewa katika kikosi cha Yanga baada ya kususa
baada ya kufanyiwa mabadiliko na Kocha George Lwandamina.
Mara
kadhaa, amekuwa akilalamika kutokana na kutopewa nafasi wakati wa Kocha
Hans van der Pluijm aliyemsajili kutoka Mgambo Shooting ya Tanga.
Hata
hivyo, kwa upande wa Lwandamina ambaye alichukua nafasi ya Pluijm,
inaonekana pia hajafurahishwa na suala lake la kususa, hivyo amemuacha
akae nje ya kikosi.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena