Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Sirro Akabidhiwa Jukumu la Mkoa wa Pwani na Mangu


Aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP), Ernest Mangu amewataka wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.
Tokeo la picha la ernest mangu
Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Ernest Mangu

Mangu amesema hayo jana Ikulu, jijini Dar es salaam baada ya Rais John Magufuli kumwapisha Simon Sirro kuwa IGP mpya wa jeshi la polisi.
Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine amesema anamfahamu Sirro kama mchapakazi mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na amani.
Alipoulizwa na waandishi wa habari wito wake kwa IGP, Sirro kuhusiana na hali tete katika wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, Mangu amesema “Sirro anafahamu anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu, ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano kumaliza matatizo yanayoendelea Kibiti na nchi nzima kwa ujumla”.
Sirro ameapishwa jana kuwa mkuu wa jeshi la polisi nhini Tanzania, kabla ya uteuzi huo alikuwa kamanda wa polisi (RPC) katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Shinyanga, Baadae alikwenda kitengo cha operesheni na mafunzo polisi makao makuu, kisha akahamishiwa kitengo hicho kanda maalumu ya Dar es Salaam kabla ya kuwa kamishna wa kanda hiyo

Post a Comment

0 Comments