Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Wazee Kituoni Magugu Wahitaji Msaada.


Na:Kennedy Lucas -Babati
Taasisi na mashirika mbalimbali yametakiwa kujitokeza kusaidia wazee wanaoishi katika kituo cha kulelea wazee kilichopo Babati Manyara kinachokabiliwa na changamoto mbalimbali.

Wito huo umetolewa na mlezi wa kituo cha kuwalea wazee kilichopo kijiji cha Sarame kata ya Magugu Babati mkoani Manyara Samson Munuo wakati akizungumza naKITUO HIKI  ameeleza  kuwa zipo changamoto nyingi zinazokikabili kituo hicho ikiwemo gari kwa ajili ya kusaidia shughuli za kituoni hapo.
Kituo hicho cha kuwalea wazee kilianzishwa mwaka 1975 wakati huo mkoa wa Manyara ikiwa ni seheem ya mkoa wa Arusha,sababu ya kuwekwa kituo katika eneo la Magugu ni kutokana na hali ya hewa ya joto katika eneo hilo inayoendana na afya za wazee.
Na hata baada ya Manyara na Arusha kujitegemea bado huduma zimeendelea kutolewa katika kituo hicho kilichopo Manyara na kinahudumia mikoa yote miwili.
Mpaka sasa kituo kinawalea wazee 13,kati ya hao 10 wakiwa ni wanaume na 3 ni wanawake.
Kituo kina uwezo wa kuchukua wazee 36 na wakati kinaanzishwa kilikuwa na hekari 65 lakini kutokana na changamoto za hapa na pale zimebaki hekari 17 baada ya serikali ya kijiji kugawa.
Kituo kipo kilomita tatu na nusu kutoka kituo cha mabasi Magugu.

Post a Comment

0 Comments