Kutokana na kuwepo kwa uvumi kuwa Mdau wa timu ya Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo’ kusema kuwa anaidai timu hiyo Shilingi bilioni 1.4 kutokana na kuingia mkataba na wadhamini wengine ambao ni Sportpesa, leo timu hiyo imetoa kauli na kuwataka wadau na mashabiki kuwa watulivu mpaka hapo zitakapotolewa taarifa za uhakika.
Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, leo kupitia app ya Simba ameandika ujumbe unaowataka wadau pamoja na wanachama wa simba kuachana na habari hizo zisizo na uhakuka na kuwa watulivu mapaka pale uongozi utakapotoa taamko juu ya mkanganyiko hUongozi utatoa tamko katika muda muafaka juu ya suala hili la muingiliano wa mkataba wa Sportpesa na uwepo wa Mo ndani ya Simba SC. Mengi yameongewa tena kwa upotoshwaji uliopitilizwa. Tuna mechi mbili mbele yetu ambazo ni muhimu zaidi kwa sasa. Tunaomba utulivu na uvumilivu wenu.
Natanguliza shukrani
Godfrey Nyange,
Makamu wa Rais.
Aidha Mdau wa Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo’ leo katika ukutrasa wake wa Twitter aliandika kuwa maesikitishwa na kitendo kilichofanywa na uongozi wa simba cha kukubali kusaini mkataba wa udhamini na Sportpesa pasipo kumshirikisha.
IT’S SAD THAT THE SIMBA LEADERSHIP HAS SIGNED A LONG TERM SPONSORSHIP DEAL WITHOUT CONSULTING WITH ME. I HAVE PUT MY BLOOD FOR THE CLUB.
— MOHAMMED DEWJI MO (@MOODEWJI).
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena