Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Rorya | Baraza la Eid Wilaya ya Rorya Lakusanya Tsh Milioni 2,679,200 kwenye Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Msikiti wa Utegi

Image may contain: sky, house, cloud and outdoor
Akifungua baraza hilo M/kiti wa CCM wilaya ya Rorya ambae aliwakilishwa na katibu wa wazazi wilaya ya Rorya ndg Furaha F Bwire, amesema anawapongeza kwa kufunga na kutimiza nguzo za kiislam na Leo kufikia hitimisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani, amesema Risala ameisoma na kusema shuguli ya ujenzi wa msikiti huu unahitaji mchanga,sementi,kokoto, nk.
Akisoma Risala ya Baraza Hilo ameelezea namna wazo la ujenzi wa Msikiti huo lilivyoanzishwa na watu wachache kwa kuanza kwa kujenga msikiti kwa nyumba ya nyasi ambao ulibuniwa na kuanzishwa na Alhaji Yusufu Sarungi Igogo ambae aliujenga mwaka 1952.
Image may contain: sky and outdoor
Alhadj Yusufu Sarungi ambae ni marehemu kwa sasa alinunua kiwanja na kuujenga kwa miti na nyasi hadi kufikia mnamo Mwaka 2002 waumini wa Utegi waliamua kufanya mabadiliko kwa ushirikiano na kujenga msikiti kwa matofari na mabati.
Katika harambee hizo za hapo jana M/kiti wa CCM Rorya Ndg. Samweli Kiboe alitoa ahadi ya sh laki tatu na nusu 350,000/= kwenye harambee hiyo.
Àkisoma risala kwa mgeni rasmi, Shehe wa msikiti wa utegi, Shehe Maulid Athumani amesema ili msikiti huu kukamilika, unahitaji jumla ya sh million 10,000,000/= Ambapo aliwashukuru wale wote waliofanikisha kwa kutoa nguvu zao na Mali zao na kuufanikisha ujenzi wa msikiti huu mpaka hapa ulipofikia M/Mungu mwingi wa rehema awabariki.
Pia katika harambee hiyo mdau mmoja ambae hakutaka jina lake litajwe ameahidi kukamilisha ujenzi wa msikiti huu hapo ulipofikia na kuukamilisha na kukabidhi uongozi funguo za msikiti huo, amewataka kumtumia picha za jengo la msikiti na garama zinazo hitajika ili aweze kukamilisha mapema iwezekanavyo.
Nae imamu wa MASJIDI NUUR kutoka Sirari Tarime Abdallah Ihonde akisoma Quraan amesema waislam na wakristo wote wanamwabudu Mungu wa mbinguni wanatakiwa kupendana na kushirikiana katika shuguli mbalimbali kama hizi za ujenzi wa msikiti na makanisa, kwani wote wanamwabudu Allah.
Image may contain: 1 person, sitting and flower
Image may contain: one or more people, people sitting, crowd and outdoor
Image may contain: 2 people, people standing
Image may contain: 5 people, people standing
Image may contain: 1 person
Image may contain: 2 people, people sitting and indoor

Picha na Kituo cha Habari na mawasiliano Rorya.

Post a Comment

0 Comments