Unaweza ukashangaa ila ndiyo hivyo kuwa Mungu ameumba viumbe wengi ambao pengine katika maisha yako viumbe wengine hutaweza kuwaona lakini sio kwa kuku aina ya Ayam Cemani ambao kila kitu kutoka kwenye miili yao ni cheusi kuanzia manyoya yao, Nyama na hadi mayai wanayototoa.
Kuku hao ambao wanapatikana kwa wingi nchini Indonessia walianza kugundulika karne ya 17 kwenye visiwa vya Java na walikuwa wakitumika zaidi kwenye imani za kidini kwa kuwaabudu kuku hao.
Kuku hao ambao hata viungo vya ndani kama ulimi, maini, utumbo na mifupa vyote vina rangi nyeusi walianza kuingia kwa mara ya kwanza barani Ulaya mnamo mwaka 1998 kwa ajili ya utafiti wa kibiolojia kwenye za Uholanzi, Ujerumani, Slovakia na Czech Republic.
Asili ya jina la kuku hao linatokana na kijiji ambacho kuku hao walianza kupatikana karne 12 yaani Ayam maana yake ‘Chickens’ na Cameni ni kijiji kilichopo kwenye kisiwa cha Java huko Indonessia.
Kwa mujibu wa mfugaji na mtalaamu wa masuala ya ndege wanaoliwa Bw. Paul Bradshaw kutoka Marekani kwenye mahojiano yake na mtandao wa Greenfire Farm amesema mayai yake yana virutubisho mara mbili ya kuku wa kawaida na pia hata nyama yake ina utofauti kidogo na kuku wa kawaida.
Hata hivyo mtaalamu huyo amesema wateja wengi wanaulizia nyama yake wengi wao wakiamini kuwa ulaji wa nyama hiyo huongeza kinga ya mwili.
Ingawaje bado hakuna tafiti zozote za kibailojia kuhusu ukweli huo mpaka sasa lakini watu wengi wa Indonesia wanaamini ulaji wa mayai mabichi ya kuku hao huondoa sumu mwilini na ni tiba kwa akina mama wanaoshikwa na uchungu wa uzazi kwa muda mrefu.
Mpaka sasa ni utafiti mmoja tuu uliofanywa na Mwanasayansi, Jan Steverink kutoka Uholanzi ambaye alibaini kuwa rangi nyeusi ya kuku hao inatokana na ongezeko la rangi kwenye tishu baada ya mabadiliko ya kijenetiki yajulikanayo kwa lugha ya kitaalamu kama (Fibromelanosis).
Kuku hao ambao wamejizolea umaarufu nchini Indonesia wamempa jina la gari la kifahari aina Lamborghini na hao wanamuita ‘Lamborghini of poultry’.
Kwa bei ya Marekani yai moja la kuku hao huuzwa mpaka dola $130 sawa na Tsh laki 2.9k, huku kuku mzima akiuzwa dola $2,500 sawa na Shilingi milioni 5.5 za kitanzania.
Swali je, unaweza ukalipia mamilioni kununua nyama ya kuku huyo? au laki tano kununua yai moja?
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena