Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Michezo | Danny Lyanga atua Mtibwa Sugar

Related image
Dar es Salaam. Achana na usajili wa kipa Shaaban Kado, Mtibwa Sugar imeonyesha msimu huu haitaki mchezo baada ya kunyakua nyota wa zamani wa Simba na Yanga, akiwamo Danny Lyanga aliyekuwa akicheza soka la kulipwa Fanja FC ya Oman.
Lyanga aliwahi kutamba Simba kabla ya kwenda Umangani na tayari amejiunga na Mtibwa sambamba na kina Kado na kiungo wa zamani wa Yanga, Hassan Dilunga aliyesaini mkataba wa miaka miwili juzi Jumapili.
Mbali na Lyanga na Dilunga, pia Mtibwa imewanasa straika wake wa zamani,  Mohammed Mkopi ambaye usajili wake kwenda Mbeya City akitokea Prisons msimu uliopita. Nyota hao walishuhudiwa wakipiga tizi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Zubeir Katwila.
"Mimi Mtibwa ni nyumbani, halafu ni sehemu ambayo imenifanya nijulikane kisoka, hivyo kusajiliwa tena sio kitu cha ajabu, ila nimerudi kuhakikisha Mtibwa inaleta mapinduzi katika soka la Tanzania," alisema Kado aliyewahi kuzidakia Yanga na Coastal Union kabla ya kutua Mwadui kwa misimu miwili iliyopita.

Post a Comment

0 Comments