Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RORYA MARA: MKUU WA WILAYA YA RORYA AKEMEA WATUMISHI WANAOHUJUMU MAPATO YA HALMASHAURI YA RORYA .

Image may contain: 3 people, people sitting and indoor
Mkuu wa Wilaya ya Rorya amekemea vikali watumishi wanaokwamisha maendeleo ya Wilaya ya Rorya kwa Kuhujumu mapato ya Halmashauri.
Akifungua baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Rorya, Mkuu wa Wilaya Saimon Kemori amekemea tabia ya watumishi ambao wamekuwa na tabia ya kukusanya MAPATO na kuweka mifukoni mwao, huku wakiwa wameaminiwa na serikali kusimamia na kukusanya mapato, lakini badala yake wamegeuka kuihujumu Halmashauri
Amewataka TAKUKURU kufuatilia na kuwachukulia hatua kwani hao in wala rushwa, haiwezekani halmashauri ikose mapato na huku watumishi wachache wakihujumu mapato.
Amesema kwanzia sasa minada bubu ambayo hufanyika kabla ya kufikisha ng'ombe mnadani ife haraka sana.na kila mfugo unaopelekwa mnadani ufike mnadani na sio kuuzia njiani na mapato kupotea.
Kuhusu Boda boda, Mkuu wa wilaya amesema kuanzia tarehe 1/7/2017 ufanyike utaratibu wa boda boda kulipa kodi ya maegesho ya vituo vya kuchukulia abiria na kufanya usajiri wa kila boda boda kujua anakaa kituo gani.
Amesema kila Boda boda atalipa mapato ya shiringi mia moja 100= tu kila siku kwa ajili ya kukusanya mapato ya halimashauri, amewataka madiwani kusimamia zoezi hill kwa kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji ili kurahisisha zoezi hili.
Katika baraza hilo kuna shirika lisilo la kiserikali la NYANJA ECONOMICS INVESTMENT TRUST FUND ambalo ofisi yao kuu imefunguliwa katika kata ya nyamunga kinesi, lilitambulisha shuguli ambazo linatarajia kuzifanya Rorya. 
Mwakilishi wa taasisi hiuo amesema taasisi hiyo inazielimishia jamii kwa ajili ya kuondokana na umasikini huku akitanabaisha shuguli wanazofanya ambazo ni:
1.uwekaji akiba katika vikundi
2.ufugaji nyuki
3.ufugaji wa samaki
4.ufugaji kuku
5.na mafunzo ya ujasiliamali.

Waheshimiwa madiwani walilipokea shirika hillo na kuwataka kuainisha ni vikundi vingapi vinatakiwa kila kijiji na kata,Dr Saganda ambae ni afisa mipango na sera wa taasisi hiyo. alisema hakuna ukomo wa vikundi katika eneo moja lengo la taasisi yake ni kuelimisha jamii na jamii inufaike na taasisi hiyo. madiwani wameitaka taasisi hiyo kufungua ofisi yao makao makuu ya wilaya ya rorya ili kuweza kufikiwa na walengwa kwa ursjisi kulingana na jiografia yarorya ilivyo.nae Dr kaganda alisema taarifa hiyo ataifikisha kwa uongozi wa juu kwa utekelezaji wa ombi hilo
Picha na kituo cha habari na mawasiliano rorya.

Msikilize Hapa Chini

Post a Comment

0 Comments