Akimkaribisha kuongea na MUJATA, mratibu wa asasi hii ya MUJATA, Peter amesema MUJATA ulianzia Mbeya kutokana na kushamiri kwa matukio yaliyo kuwa yanajitokeza ya mauwaji,ujambazi na kuunda muungano huo wa mujata na kuleta Amani katika MKOA wa Mbeya .
RPC MWAIBAMBE Akishukuru wana mujata kwa muungano wao ambao umepelekea Tarime na Rorya kuwepo kwa Amani kama risala ya mujata inavyo sema, amewataka wananchi kupitia muungano huu wa mujata kushirikiana na ofisi yake kwa ajili ya kuendelea kupatikana kwa Amani katika mkoa wa kipolisi wa tarime/rorya. Amesema Amani inapatikana kama ushirikiano baina ya jamii na vyombo vya dola unapo kuwepo. Amesema bila ya wananchi kushirikiana na polis ufanisi wa matazo kwa jamii hauwezi kupatikana. Amepongeza kwa wazee wa koo13 za kabila la wakuria kuungana na kuwa kitu kimoja na kusema huo in mwanzo mzuri wa kupunguza matatizo yanayo kuwa yana jitokeza ndani ya jamii.
Amewataka viongozi wa mila kumpa ushirikiano ili kuweza kusaidiana katika nyanja zote zinazo husu jamii.katika kuleta Amani kati ya jamii na vyombo vya dola.amewataka wana mujata kumpigia simu wakati wowote pale wanapo hitaji ushauri na msaada wake katika chombo hiki muhimu cha jamii.ameahidi kuita viongozi wa mujata na kufanya mazungumzo nao kwa ajili ya kuendeleza chombo hiki.na kutafuta namna ya kutafuta wafadhili watakao weza kukisaidia chombo hiki ili kiweze kufikia malengo yaliyo kusudiwa.
Picha na kituo cha habari na mawasiliano rorya.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena