Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | Uhalisia kuhusu Dhana ya Mauaji ya Kimbari

Image result for rwandan genocide
Msamiati wa "mauaji ya kimbari" ( Genocide) ni msamiati ambao tumekuwa tukiusikia Mara nyingi tu hasa kwenye vyombo vya habari na Mara nyingi unapotamkwa msamiati huu basi itakuwa inazungumziwa nchi ya Rwanda kutokana na madhira yaliyowakuta mwaka 1994 ambapo zaidi ya watu 800,000
walipoteza maisha wengi wao wakiwa Watutsi pamoja na baadhi ya Wahutu wenye msimamo wa wastani! Haya yalikuja kufuatia kifo cha utata cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo bwana Juvenal Habyimana na mwenzake Cprien Nyadyamila wa Burundi baada ya ndege yao kudunguliwa wakati ikitua kwenye uwanja wa Kigali ikitokea jijini Dares Salaam Tanzania! Au watakuwa wanazungumzia vifo vya wayahudi million 6 waliouliwa na Adolf Alois Hitler wakati wa vita kuu ya pili, japo wapo wanaoliukiza wayahudi million 6 Hitler aliwatoa wapi! Au watakuwa wanaizungumzia vita ya  Kossovo kipindi cha bwana Slobodan Milosovic akiwa Rais wa iliyokuwa Yugoslavia( sasa Serbia na Herzegovina, Latvia na nyingine nyingi)!
 
Image result for rwandan genocide
Lakin je msamiati huu tunaelewa katika mazingira yake kiuhalisia! Basi naomba kushare kidogo kuhusu msamiati huu na unamaniisha nini hasa katika ulimwengu wa sheria za kimataifa na wabobezi wa mambo hayo.

Image result for rwandan genocide
Kwanza kabisa niweke wazi mauaji ya kimbari ni mojawapo ya makosa yanayopatikana kwenye mkataba wa kimataifa unaoanzisha mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai "ICC" wa the 'Rome Convention"  na kwenye 'The Statute of the international Criminal Court"! Na ni kosa ambalo mtu yeyote kutoka nchi yeyote anaweza kushitakiwa katika nchi yoyote japo,  ICC kimsingi ndo imepewa mamlaka hayo.
Sasa mauaji ya kimbari ( genocide) ni nini!?

Kama nilivosema mwanzo wengi wetu tunaposikia mauaji ya kimbali basi moja kwa moja huchukulia kuwa ni mauaji yanayohusisha kuuawa kwa watu wengi kwa wakati mmoja! Lakini kiuhalisia hiyo si tafasiri sahihi.

Kiufundi mauaji ya kimbali ni pale mtu, watu au kikundi Fulani cha  cha watu kinapoamua kuwaua watu Fulani  ambao wana uhusiano katika namna moja au nyingine kwa lengo la kuhakikisha wanafutika kwenye uso wa dunia.
Uhusiano huu unaweza kuwa ni wa kikabila, kidini, kisiasa au namna yoyote nyingine ile.


Hivyo basi ili tukio fulani la mauaji liweze kupewa hadhi ya mauaji ya kimbari ni lazima;

1. Wauawe watu wanaohusiana juu ya jambo fulani la kufanana (hao wanao uwawa).

2. Wauaji lazima wawe na lengo la kutaka kuungamiza kabisa kundi hilo kutoka kwenye uso wa dunia.                      
Sasa ukiangalia hapo juu ni kwamba hakuna sehemu wanasema au wanaweza kigezo cha idadi ya watu waliouawa ila kufanya tukio fulani kuwa mauaji ya kimbari au hapana!

Kwa lugha nyingine hata mauaji ya watu wawili kuna kipindi yanaweza kuwa mauaji ya kimbali kama yatakuwa yanaingia katika mlengo nilioueleza hapo juu!

Mauaji ya wayahudi yalilenga kuhakikisha jamii hiyo inafutika kabisa,  mauaji ya Rwanda yalilenga kuhakikisha jamii ya kitutsi inafutika kabisa nchini Rwanda.


Kosa la mauaji ya kimbali linaweza kufanyika kwa njia ya ubakaji!

Katika moja ya kesi za mauaji ya kimbali ya Rwanda ilielezwa kuwa kosa la mauaji ya kimbali( genocide) linaweza kufanyika kwa njia ya ubakaji!

 Kwa mjibu wa hoja hii wanawake ndio chanzo kikuu cha uzazi duniani hivyo ubakaji unaweza kutumika kama silaha ya mauaji ya kimbali!! Kwa mfano wanaume wa  kabila "X" wanaamua kuwabaka wanawake wa kabila "Y" katika ubakaji huo wanaweza kutokea mambo mawili au matatu!

1. Wanawake waliobakwa wakabeba ujauzito, sasa basi asilimia 99% ya  waafrica tunachukua kabila la baba, kwahiyo hawa wanawake watakapojifungua basi watoto wale watachukuliwa kuwa ni kabila "X" hivyo watakuwa wamefanya kabila "Y" litoweke kwenye  uso wa dunia huku wakilifanya kabila "X" liendelee kutamalaki!

2. Kisaikolojia mwanamke anapobakwa basi huchukia wanaume na tendo la ndoa, hivyo wanaume wa kabila "X" wanapowabaka wanawake wa kabila "Y" wanaweza kuwafanya wanawake hawa wachukie tendo la ndoa au wawachukie wanaume wengine wote hata wa kabila lao, na hii inaweza kupekekea kutoweka kwa kabila "X" kwa kuwa wanawake wa kabila hili hawatweza  tena kuzaa maana wanachukia tendo la ndoa na  wanaume kwa ujumla.

Ni ajabu lakini ni moja ya hoja ambazo ilimpeleka mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya kimbali ya Rwanda jela!

Sasa basi baada ya hayo machache hapo juu tunaweza kuhoji na kujiuliza maswali kadhaa;

1. Je, tunaweza tukasema mauaji ya Albino yaliyotamalaki Siku za nyuma hapa nchini Tanzania yalikuwa mauaji ya kimbari ( genocide)?

2. Au mauaji ya wazee vikongwe huko kanda ya ziwa yanaweza kuwa mauaji ya kimbari genocide)!?

Ikumbukwe kuwa makosa ya  mauaji ya kimbari na 'uhalifu dhidi ya ubinadamu' yanaweza kufanyika wakati wa amani kukiwa hakuna vita au vita ikiwepo. Lakini kosa la uhalifu wa kivita ndilo sharti kuwe na vita.


Asante
Credit Goes To H.E The Bold

Post a Comment

0 Comments