Waandaaji wa tuzo za Vijana Afrika wametoa majina ya vijana 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika kwa mwaka 2017.
Katika listi hiyo Tanzania imeingiza vijana nane ambao ni Ali Kiba, Elizabeth Michael, Flaviana Matata, Diamond Platnumz, Lilian Makoi, Jokate Mwegelo, Nancy Sumari na Millard Ayo.
Vigezo ambavyo vimetumika ni pamoja na umri kuanzia miaka 40 kushuka chini, kuwa na uwezo wa kuishawishi jamii na haikuhusisha kiwango cha mtu cha elimu.
Isome listi kamili hapa chini.
Mastaa wa Bongo Fleva kutoka Tanzania, Alikiba na Diamond Platnumz wametajwa kwenye orodha ya vijana 100 waliochini ya miaka 40 wenye ushawishi zaidi barani Africa kwa mwaka 2017.
Kwenye orodha hiyo iliyotolewa leo na mtandao wa African Youth Awards imemtaja pia muigizaji wa filamu nchini Tanzania mrembo Elizabeth ‘Lulu’ Michael na mwanamitindo Flaviana Matata kwenye orodha hiyo ya vijana 100 wenye ushawishi zaidi barani Africa.
Kwa upande mwingine wasanii waliochaguliwa kwenye orodha hiyo kutoka nje ya Tanzania ni Davido kutoka Nigeria , Rapa AKA kutoka Afrika Kusini na wengine wengi.
Dirisha la kupendekeza majina ya vijana wenye ushawishi zaidi barani Afrika mwaka 2017 lilifunguliwa mwezi June 25 na kufungwa agosti 22 mwaka huu.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena