Abdallah Twalipo Julius Nyerere na Mirisho Sarakikya |
Sasa jukumu la msingi la kurejesha mipaka ya nchi likawa limekamilika na Rais Julius Nyerere akaja kule na akasimama eneo lenye kilima pale na tukamweleza kwamba sasa mzee kazi ya kwanza uliyotutuma tumeimaliza, mipaka yetu sasa iko salama, akasema vizuri lakini huyu “mshenzi” huyu ametuharibia mambo mengi sana si bado yuko kule (nchini mwake), basi kazi bado haijakwisha.
Ndipo tukaingia hatua ya pili, maana sehemu ya kwanza ya ukombozi wa nchi yetu ikawa imekwisha ikafuata hatua hiyo ya pili ambayo ni kumwadhibu adui". OPERATION YA JESHI LETU NDANI YA UGANDA. "Pale kilichofanyika ni kwamba baada ya kumaliza ile kazi ya awali, tukaingia sasa kazi ya kuandaa na kutekeleza operesheni ya kuvuka mpaka ambayo ni tofauti na opereshani ya kumwondoa adui nyumbani kwako.
Sasa unakwenda nyumbani kwake lazima uwe na mkakati, sambamba na nguvu ya kutosha kwenda kwake, kwa hiyo rais ikabidi afanye utaratibu wa kumtafuta kamanda wa kuingia Uganda, mimi si ndiye niliyekuwa Chief of Staff na mkuu wa majeshi akiwa Twalipo ambaye naye hayuko makao makuu, kwa maana hiyo akiwa huku mbele (vitani) kule makao makuu hakuna maandalizi yoyote, nani anaanda nini nani anafanya nini.
Kwa hiyo ilibidi nirudi Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam na pale (vitani kuelekea ndani ya Uganda) nikamkabidhi Msuguri, mimi nikamwambia nakwenda (makao makuu) kukufanyia kazi ya kuandaa vifaa, wewe kazi yako ni kwenda ndani kumwadhibu Idi Amin.
Nikarudi makao makuu nilikuwa na mtu mmoja alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi, Kanali Bakari, basi tukafanya kazi na Bakari, tukaenda hadi nchi za nje kutafuta nguvu, zana za kivita.
Wako marafiki walitusaidia, sina sababu ya kuwataja sana lakini kati ya nchi rafiki tulizokwenda ni pamoja na Urusi, China, Korea na Bulgaria.
Ikabidi tukusanye vifaa na ndipo hapo wananchi walichangia mambo mengi sana.
wapo waliojitolea magari yao, vyakula, mifugo kama ng’ombe ili kuwawezesha wapiganaji wetu kule mstari na hatimaye Msuguri akuvuka mpaka akiwa na uhakika wa nguvu za kutosha na uangalizi huku nyuma anakotoka ". UDHIBITI WA UVUJAJI WA SIRI. "Kwanza wakati nikiwa pale Kagera tulikuwa tumedhibiti sana uvujaji wa taarifa.
Unajua kuna mkutano mmoja mkubwa wa kimataifa ulikuwa unaendelea pale Arusha uliokuwa umehusisha nchi nyingi huku vita pia ikiendelea na hao washiriki wa mkutano hawakujua chochote kilichokuwa kikiendelea nilidhibiti uvujaji wa taarifa, viongozi wengine tuliwapa amri maalumu hakuna kufika kwenye eneo la vita na wala kupewa taarifa yoyote.
Ni kama tulivyokuwa tunapambana kuwasaidia kule Msumbiji siku moja tukakuta mzee mmoja wa kizungu kule Tunduru anayo redio ameijichimbia ndani, kumbe alikuwa anawasiliana kwa maana ya kupeleka taarifa, tukamkamata.
Hata pale Karagwe, tulikuwa na watu fulani pale ambao ni kanisa fulani sitaki kuwataja nao pia walikuwa na redio ya mawasiliano, ukiona utafikiri mtu anapiga kinanda kumbe anapeleka taarifa, kwa hiyo tukafunga njia zote za mawasiliano, nikasema hakuna mawasiliano ya aina yoyote na taarifa zozote kwenda Ikulu nitapeleka, tulihakikisha taarifa hazivuji vinginevyo tusingeweza kuvuka pale." MCHANGO WA MUSEVEN.
Museven yeye alitokea huku nyuma kapitia Karagwe kalala kijijini pale wakati Mayunga amekwishavuka mpaka, akaungana na Mayunga, ukweli ni kwamba Jeshi la Tanzania na chini ya Luteni Jenerali Mayunga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya kupita Mbarara na kutoka hapo kuelekea Kampala, na wengine wakapita Minziro kwenda kuungana kule.
Museven hakuwa na jukumu la kuongoza ni kama alisaidia mambo kadhaa yakiwamo masuala ya taarifa.
NINI KILIENDELEA BAADA YA VITA. "Baada ya vita, tukawapokea vijana kutoka Uganda pale Bunazi, nikafanya kazi ya kuwasambaza na kuwarudisha kule walikotoka, wengine Ruvuma, Kigoma na maeneo mengine ya nchi. Tukahakikisha wamerudi na kupewa haki zao.
Baada ya kumaliza pale Bunazi, nikarudi Dar es Salaam kwenye kitengo changu cha Mnadhimu Mkuu, sasa makamanda wote wakawa wamerejea kutoka vitani.
Ikabidi sasa jeshi lipangwe upya, unajua watu walikwishaonja kutoa roho za watu huwezi kucheza nao hivi hivi, ikabidi sasa tupangane upya.
Namna gani jeshi litakavyoendeshwa na kwa hiyo, Amiri Jeshi Mkuu akapanga upya akasema "sasa wewe bwana umemaliza kazi hii nakushukuru, sasa nataka kukupa kazi nyingine", nikamwambia "sawa, nipo tayari kwa kazi yoyote", akaniambia "utakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga", nikamwambia "naenda lakini hii kazi sijawahi kufanya sasa ukiona nafanya vibaya uniite, na mimi nikiona kuna tatizo nitakuja". Kwa hiyo nikaenda zangu Tanga ndipo wakati huo yakafanyika mabadiliko, Twalipo akatoka pale akawa Waziri wa Ulinzi, Msuguri akawa Mkuu wa Majeshi halafu na Jenerali Kombe akawa Mnadhimu Mkuu ". Huo ndo ukawa mwisho wa simulizi ya oparesheni ya vita ya kagera, jenerali kiwelu mpaka Leo hii yuko hai bado, Msuguri tayari ameshafariki kwa maradhi ya kawaida. Twalipo yeye bado yuko hai kama ilivyo kiwelu na jenerali kombe huyu aliuwawa kwa kupigwa risasi nne kifuani na askari polisi na mauaji yake yalileta utata sana mpaka Leo hii. Kesho ntaleta simulizi ya mauaji yake jenerali IMRAN KOMBE na utata wake na wahusika wake na mazingaombwe ya kupigwa bao la mkono na ......... Cjamalizia kwasababu za kiusalama..!!!! Kwa hiyo picha ya kiwelu amabayo yuko kwenye kikao cha CCM mtaniwia radhi kama ntamkera mtu kutokana na sare za chama zilizoonekana imenibidi kutokana na uhaba wa picha za Kiwelu...!!!!! MWISHO....!!!!!!
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena