Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RORYA MARA: MWENGE WA UHURU WILAYANI RORYA WAZINDUA MIRADI MBALIMBALI NA MINGINE KUWEKA MAWE YA MSINGI.

Mkuu wa wilaya ya Rorya Mhe. Saimoni Kemori Chacha akimkaribisha kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndg kufungua kiwanda cha kuchambua na kupanga madaraja mchele cha Irienyi, amewapongeza wakimbiza mwenge kitaifa na Mkoa kwa jinsi walivyo tembelea miradi mbali mbali na kujionea shuguli na miradi iliyo tekelezwa kwa nguvu za wananchi,serikali na wahisani.

Miradi ikiwemo kuzindua ward ya wazazi kituo cha afya kinesi, Hifadhi ya mazingira G.R.A kinesi, Skimu ya umwagiliaji irienyi ,kuzindua kiwanda cha kuchakata na kupanga madaraja kiwanda cha Mchele irienyi, kukagua ujenzi wa Barbara Irienyi Baraki, Kuteketeza bangi na madawa ya kulevya viwanja vya Osogo utegi, Kufungua madarsa 4 jengo la utawala na matundu 10 ya vyoo shule ya sekondari Nyamtinga na kufunguliwa shule mpya ya msingi Nyang'ombe.

Amesema maelekezo yaliyo tolewa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Kimori amemwambia yeye na viongozi wengine waandamizi wa wilaya watafayia kazi kasoro ndogo zilizo jitokeza na kuhakikisha Rorya inaendelea kufanya vizuri. Kuhusu upimaji wa Afya ya maleria, vvu na utoaji Damu, Mkuu wa wilaya Kemori amesema.wananchi walio jitokeza kwa hiari yao kupima vvu ni 609 na kati yao wanaume walio Pima ni 450 na kati yao waliopatikana na maambukizi ni 17 na wanawake waliojitokeza kupima ni 198 na waliokutwa na maambukizi ni 10 sawa na 4% ya walio jitokeza kupima.
Kuhusu maleria waliojitokeza kupima kwa hiari ni 384 kati yao wanaume ni 203 nawaliokutwa na maleria ni 34, na wanawake walio Pima ni 198 waliokutwa na malaria ni 19 sawa na 19.8 ya walio Pima maleria.kuhusu uchangiaji wa Damu salama mkuu wa wilaya Kemori amesema zilipatikana chupa 19 za Damu hawa ni wananchi walio jitokeza kupima kwa hiari yao wenyewe.pia mkuu wa wilaya Kemori amemweleza kiongozi wa mbio za mwenge kwamba kama alivyo jionea katika mabanda mbali kulitolewa elimu mbalibali kwa zaidi ya watu 128 na kutolewa vipeperushi juu ya mpango wa uzazi.na kuhusu dawa za kulevya watu 230 walipata elimu juu ya athari ya matumizi ya madawa ya kulevya na madhara yake.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndg Amour Mohamed Amour amesema amezunguka mikoa 22 na kuzindua miradi mbali mbali, lakini wananchi wa Rorya wametekeleza shuguli za Maendeleo kwa vitendo, Hasa pale wanapotumia nguvu kazi kwa pamoja na kuibua miradi ambayo inapelekea serikali kuunga mkono shuguli zao! Alipongeza sana kikundi cha kilimo cha irienyi kwa kuwa na shamba kubwa la skimu ya umwagiliaji na kwamba uanzishwaji wa kiwanda cha kuchakata na kupanga madaraja ya mchele kitawanufaisha wengi na kutoa ajira nyingi kwa vijana.pia kitaleta uwiano kati ya maeneo mengine na kuleta Maendeleo katika wilaya ya Rorya, pia miundombinu ya Barabara itaboreshwa kwa sababu ya kuwepo kwa uchumi wa viwanda.
Ameahidi kumfikishia Rais Magufuli kwamba wilaya ya Rorya inakuunga mkono kwa swala zima la kusimamia na kutekeleza kauli mbiu yake ya Tanzania ya viwanda Rorya inawezekana.
Mwenge wa Uhuru ulimaliza mbio zake wilayani Rorya na kukabidhiwa wilaya ya Tarime saa 3 asubuhi ili kuendelea na mbio wilayani Tarime.

Kituo cha Habari na Mawasiliano Rorya.

Post a Comment

0 Comments