Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Mahusiano | Upweke ni Mbaya Ila Mapenzi Nayo ni Full Stress

Image result for BLACK COUPLE
Mpenzi msomaji ni siku nyingine Mungu ametujalia kukutana katika kuelimishana juu ya maisha ya uhusiano kupitia safu yetu nzuri ya XXLove. 

Kama ambavyo mada inajieleza hapo juu, mapenzi ni ya ajabu sana. Kuna baadhi ya watu wanateseka kwa sababu wana upweke, lakini wakati huohuo baadhi ya watu walio kwenye uhusiano wao wanateseka kwa sababu ya ‘stresi’ za wapenzi wao.
Wakati wewe ukiteseka kwa kutokuwa na mtu wa kukufariji na kukushauri kuhusu maisha, mwingine aliye na mtu huyo anateseka kwa sababu anahisi mtu wake si mwaminifu, hana upendo na akili ya maisha.

Ni kweli mapenzi yanatesa na kuumiza, lakini cha ajabu kuna watu wanatamani kuingia kwenye mapenzi hayohayo ingawa na walio kwenye uhusiano wanatamani kutoka kwa sababu ya kuchoshwa na stresi za wenza wao.

Maana yangu ni kwamba, mtu aliye mpweke anapata wakati mgumu kwa sababu kuna muda anatamani kuwa na msaidizi, lakini kwa sababu zake binafsi anashindwa kufikia muafaka.
Wakati huohuo, kuna mwingine ana mwenza wake, lakini kila kukicha yeye ni mtu wa mawazo (stresi), anaona kama mwenza wake ni msaliti, mfujaji, bahili, hana msaada wowote katika maisha yake.

Kama mwanadamu, ni kweli, kuna muda unatamani kuwa na mtu, lakini ukikumbuka kile kilichotokea kwenye penzi lako la nyuma, unajikuta moyo unakufa ganzi. Aidha, kwa sababu ya kutendwa au kwa kuachwa au kutelekezwa na mtu uliyempenda na kumthamini sana katika maisha yako.
Upweke ni mbaya na unaua. Wakati mwingine kuna mambo ambayo unatamani kuyafanya au unahitaji msaada wa mwenza wako, lakini ukiangalia upande wa kitanda chako unakuta uko peke yako. 

Inawezekana unakutana na changamoto ngumu zaidi ambayo unaamini kama ungekuwa na ubavu wako, basi ungepata suluhu.
Kuna wakati unahitaji ushauri kwa sababu ya jambo f’lani, moyo wako unatamani kabisa kumshirikisha mtu mwingine, lakini unamkosa mtu huyo.
Kwa mtu ambaye yuko kwenye uhusiano, naye kuna wakati anatamani ajinasue kwa sababu kila siku ni makwazo, machukizo na hisia mbaya.

Aidha, mpenzi, mchumba au mume wake anatembea na mama mwenye nyumba, dada wa kazi au mfanyakazi mwenzake.
Ni kweli uhusiano una stresi sana, hasa kama mlio kwenye uhusiano mtakuwa si waaminifu au mmoja wenu ni mwaminifu na mwingine hajatulia.
Mfano; mpenzi wako akichelewa kurudi nyumbani kutoka kazini unaanza kuhisi labda amepitia kwa mwanamke mwingine. Ukipiga simu ikachelewa kupokelewa au ikawa inatumika kwa muda mrefu, inakuwa ni tatizo! 

Unawaza labda anazungumza na mchepuko wake. Yaani ni fulu stresi, muda wote mwenza wako akiwa bize na kuchati unawaza labda anachati na mchepuko.

Post a Comment

0 Comments