Uwanja wa Klabu ya Barcelona unatarajiwa kubadilishwa jina la la sasa la ‘Nou Camp’ na kuitwa ‘Nou Camp Grifol’ kuanzia msimu ujao wa ligi 2018/2019.
Miamba hao wa soka nchini Hispania wamekubali kubadilisha jina hilo baada ya kusaini dili na kampuni inayohusiana na masuala ya madawa na kemikali iitwayo Grifol ambapo dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya kiasi cha £340m.
Mkataba wa Kampuni ya Grifol na Barcelona utawafanya Grifol kulipia marekebisho ya uwanja wa sasa wa Barcelona .
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Radio Marca ya nchini Hispania zinasema kuwa Kampuni ya Grifol watatoa kiasi cha £535m kwa ajili ya upanuzi na maboresho ya uwanja huo wa Nou Camp.
Hata hivyo, gazeti la Marca la nchini humo limeeleza kuwa huenda dili hilo likaongeza nguvu ya kumbakisha mshambuliaji wao Lionel Messi kuongeza mkataba baada ya taarifa kuwa klabu ya Manchester City imetenga kiasi cha Euro milioni 400 ili kumng’oa klabuni hapo.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena