Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Espionage | Ubelgiji - Kijiwe Maarufu cha 'SPIES' Duniani

Image result for espionage
f9eb37821dc7665cdaa1a266c33c1ac9--jets-smooth.jpg

Dunia yetu ina mambo mengi ya asili na yasiyo ya asili ambayo yamefanya kuwa sehemu muafaka kwa binadamu kuishi na kuendesha maisha yake. Vitu hivi kwa ujumla wake vimefanya maeneo tofauti tofauti kuwa na sifa tofauti tofauti na kuwavutia binadamu kwenda kuishi au kutembelea maeneo hayo ama kwa kupenda au kulazimika kutokana na mahitaji tofauti tofauti kuanzia ya kibifisi hadi ya kiinchi.

Moja ya vitu hivi ni majiji mazuri mazuri kuanzia majiji ya biashara kama vile New York, au yale ya starehe kama vile Los Angels au Paris, au labda majiji ya kitali na kibenki kama vile Geneva au Zurich na huku kwetu tunaweza kujikakamua kwa kutaja jiji la Arusha kama jiji la kitali.

Lakini pale Ulaya kuna jiji moja amabalo pamoja na mambo mengine limejizolea sifa ya kuwa jiji lenye shughuli nyingi za kijasusi, hili ni jiji la Brussels mji mkuu wa taifa la ubelgiji.

Mtaalamu mmoja wa mambo ya ulinzi anaweka wazi kuwa Brussels ni moja ya maeneo ambapo ni rahisi kukutana na spies kutoka karibu kila kona ya dunia na anasema kwakuwa ni sehemu ambayo wanalazimika kuwepo.

*Nini wanachotafuta*

Kama nilivosema hapo juu watu wamekuwa wakivutiwa kwenda kuishi au kuzuru eneo fulani la dunia ama kutokana na maslahi binafisi au yake ya kiinchi, kwa Brussels wengi wa wageni hawa hawa wanalazimika kufika hapo kutokana na maslahi ya kiinchi na hii inatokana na sababu kadha wa kadhaa.

Kwa mfano;

*Uwepo wa Umoja wa Ulaya*
Brussels ndio makao makuu ya Umoja wa Ulaya na taasisi kadha wa kadha za Umoja huo likiwemo bunge la ulaya zinapatikana hapa. Hii maana yake ni kuwa maamuzi makubwa yote kuhusu Umoja huo kufanyika hapa na kama tunavyojua hili ni moja ya mabara ambayo yamepiga hatua kubwa ya maendeleo katika nyanja zote hivyo chochote wanachokiamaua basi lazima angalau kila pembe ya dunia kwa namna Fulani iguswe na kwa msingi huo kila taifa linajitahidi kuhakikisha linaweka sikio lake katika eneo hilo na hapa ni mataifa yote yakiwemo ya Ulaya na marafiki zao kama vile Marekani, moja ya taasisi ya kijasusi ambayo imekuwa ikisemekana kuweka watu wake wa kutosha ni M16.

*Makao makuu ya NATO*
Hii ni sababu nyingine, uwepo wa NATO unafanya mataifa kadha wa kadha kutaka kuhakikisha wanajua kile kinachopangwa, kuratibiwa au kuwekewa mikakati na NATO. Kama tunavyojua muungano huo umekuwa muhimili muhimu kwenye mambo ya kiulinzi ya mataifa ya Ulaya na Marekani lakini pia muungano huo umekuwa ukileta changamoto kwa mataifa kama Russia, China, Iran na mataifa mengine mengi. Kwahiyo kwa vyovyote vile lazima waweke watu hapa ili kujua kile kinachotokea.

*Brussels ni mji wa watatu duniani kwa kutokea mikutano mingi ya kimataifa*
Hii maana yake ni kwamba hapa ni moja ya sehemu ambapo mipango mingi na maamuzi makubwa makubwa kuhusu mienendo ya dunia katika masuala yote inapangwa na kuamuriwa, ni kwa msingi huo basi mashirika ya kijasusi kutoka mataifa kadha wa kadha yanahakikisha maskio yao hayabanduki katika jiji hili ili kujua A B C D ya kile kinachojadiliwa.

*Mji huu unasemekana kuwa na idadi kubwa ya mabalozi na waandishi wa habari*
Katika ulimwengu wa kisasa wa masuala ya kijasusi kwa kivuli cha diplomasia, waandishi wa habari na wanafunzi inasemekana ni njia bora zaidi kabisa ya kupenyeza spies katika eneo husika. Sasa basi Brussels kama makao makuu ya Umoja wa Ulaya imejikuta ikipokea wanadiplomasia na waandishi wengi sana ambapo humo ndio spies wanakojificha na kufanya mji huo ufurike wazee hao wa kazi.

*Wanakuja katika sura zifuatazo*

- Kama wanadiplomasia

- Kama waandishi wa habari

- Kama wanafunzi

- Kama malobbysit ambapo hadi mwaka 2009 kulikuwa na zaidi ya makampuni 286 yaliyosajiliwa kama lobbying Consultancies.

- Wafanya biashara

Ukiacha kufanya shughuli za kipelelezi watu hawa pia hujaribu kuinfluence maamuzi ya yanayofanywa na maafisa wengine, inasemekana watu hawa hujaribu kuanzisha mawasiliano na maofisa wa EU kupitia semina na matukio ya kijamii. Taarifa zinazotafutwa zinategemeea nchi na nchi kwa mfano Russia wanakuwa tafuta sana habari kuhusu mawasiliano, Sera za kiulinzi na mambo ya counterintelligence huku wachina wao wakiwa wanatoa macho sana kwenye taarifa zinazohusiana na mambo ya kiuchumi na masuala ya tecknolojia cha ajabu ni kuwa wale wa Iran wanatumia muda mwingi kuwapeleleza mabolozi na wanadiplomasia wa nchi hiyo.

Lakini kama nilivosema mwanzo si Mataifa shindani tu na Ulaya yanayofanya ujasusi mjini Brussels bali hata mataifa rafiki yamo hasa katika masuala nyeti yanayohusisha uchumi na Sayansi basi kila idara ya Usalama hujikutakatika ushindani na idara zingine
*Warusi huwa hawalazi damu*

Kama inavyofahamika Warusi wamekuwa washindani wa Jumuiya ya Ulaya na Marekani kwa muda mrefu tunaweza kusema hata NATO inaweza kuwa iliundwa pamoja na mambo mengine kuhakikisha inazilinda nchi za muungano dhidi ya Urusi hivyo basi kila wanapokuwepo watu wa Jumuiya ya Ulaya au NATO basi Warusi lazima wahakikishe wanakuwepo mahali hapo.

Sasa mwaka 2009 mtu mmoja kwa jina la Simiin raia wa Estonia na ambaye alikuwa afisa wa wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo anayehusika na ubadilishanaji wa nyaraka mhimu na EU alifungwa jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya kazi na Warusi. Huyu jamaa alikuwa ni moja ya watu waliokuwa wakihudhuria semina na makongamano mengi ya EU hapo Brussels. Alituhumiwa kuwa na mawasiliano na Vasily Chizhov mtoto wa balozi wa Urusi Umoja wa Ulaya bwana Vladimir Chizhov na inasemekana 'handler' wake alikuwa MTU mmoja akiwa chini ya kivuli cha mfanya biashara na akiwa na uraia wa Ureno. Baada ya tukio hili bwana Vladimir Chichov na mwanawe walifukuzwa kutoka Brussels.

Kwa miongo kadhaa ijayo Brussels itaendelea kuwa kitovu na 'kijiwe' maarufu cha 'spies' katika nyanja za kimataifa.

Post a Comment

0 Comments