Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Fahamu | Nguvu ya mapenzi katika kufanikiwa

Image result for loveKazi yangu kila Jumapili ni kukuletea nukuu saba kutoka kwa watu ambao wamefanya mambo makubwa au ya kipekee katika ulimwengu huu. Nukuu za leo zimejikita katika upendo au mapenzi (love) kama sehemu ya kukufanya kuwa bora zaidi kuelekea mafanikio.1. Si kwa kiwango gani tunafanya, bali ni upendo wa kiasi gani tunauweka katika kile tunachofanya. Haijalishi tunatoa kiasi gani, bali tunatoa kwa upendo wa kiasi gani – Mother Teresa.
2. Ni kitu gani chenye nguvu zaidi ya upendo? – Igor Stravinsky.
3. Mara nyingi maisha huja kupitia upendo wa kipekee – Elbert Hubbard.
4. Aliyefikia mafanikio aliishi vizuri, alitabasamu mara kwa mara na alipenda sana – Unknown.
5. Upendo ni maisha…. na iwapo utakosa upendo, utayakosa maisha – Leo Buscaglia.
6. Kadiri unavyojifunnza kupenda, ndivyo unajifunza namna ya kuishi – Unknown.
7. Maisha bila upendo ni sawa na samaki bila bahari, ni kama anga bila nyota, na hata mwili bila roho – Delno L. A. Tromp.
Shukrani, dondosha comment yako hapo chini kuelezea ni nukuu ipi imekubamba zaidi.

Post a Comment

0 Comments