Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Makala Maalum | BLACK WEDNESDAY: Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na Yaliyo Nyuma ya Pazia

Image result for FOREX


Nimekuwa nikiepuka kuandika chochote kuhusu Forex ili kuepuka kuonekana naipigia debe (kama nikiandika positively) au labda "natia mchanga kitumbua" cha watu (kama nikiandika negatively).

Lakini baada ya tafakari ya kina na utafiti, nimeonelea nitie mkono kuandika yale ninayoyajua juu ya biashara hii na masuala kadhaa ambayo naamini labda watu wengi (pengine hata wale wanayoifanya) hawayajui.

Hiki ninachokiandika hapa ni visa vya kweli na matukio halisi ambayo yametokea. Majina yote ni ya watu halisi isipokuwa sehemu chache ambazo nimebadili majina kidogo ili kulinda identity za wahusika.

Saa 23:40, Kituo Cha Polisi Oysterbay

Sikumbuki ni muda gani halisi kabisa nilifika mahali hapa lakini kwa kumbukumbu ya haraka nakadiria kwamba ilikuwa yapata kama saa sita kasoro usiku nilifika Kituo cha Polisi Oysterbay. Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 6, October mwaka huu 2017.

Pale "getini" kwenye ukaguzi nilimkuta askari fulani ambaye tunafahamiana kiasi.

"Meja niazime sweta..!" Nilimuomba sweta huyu askari ambaye mara nyingi huwa tunaitana jina la utani la "Meja".

Kutokana na udharura wa simu ambayo nilikuwa nimepigiwa, niliondoka nyumbani kama nilivyo. Nilijisahau kubadili tisheti ambayo nilikuwa nimeivaa. Ilikuwa ni tisheti fulani hivi ya 'combat' ya jeshi la Navy la Marekani. Mara nyingi nikiwa nyumbani huwa napendelea kuivaa hii tisheti. Sasa kutokana na eneo husika (kituo cha Polisi) sikuona busara ya kuingia na "combat ya kijeshi" japo haikuwa ya nchi yetu lakini pia sikutaka attention za watu kuwa kwangu nikiingia humu kituoni.

Nilikuwa natembea kutoka pale getini kuelekea kule kwenye kituo chenyewe huku kichwani nikipiga hesabu ni namna gani au kitu gani naweza kufanya kwa namna ya changamoto iliyo mbele yangu.

Nikatembea mpaka mbele ya mlango wa kuingia kituoni.. kwa wale wanaopafahamu pale mbele wamejenga kama 'balcony' hivi za zege, nikasimama hapa kwa karibia dakika tano nzima. Japokuwa huwa hawaruhusu kusimama hapa muda mrefu kwa sababu za kiusalama lakini nahisi lile sweta ambalo aliniazima 'Meja' pale getini kwa kuwa lilikuwa sweta la kipolisi (yale masweta ya rangi ya zambarau) nadhani ndio maana hakuna askari aliyeniuliza chochote kwa muda wote huu ambao nilikuwa nimesimama hapa.

Nilikuwa nasita kuingia moja kwa moja mpaka 'kaunta' sehemu ya Maulizo kwa kuwa sikuwa nimeafikiana na akili yangu ni namna gani nitaenda kuongea. Kwa hiyi nikaendelea kusubiri kigodo nikiwaza na kuwazua kitu cha kuongea.

Nikiwa katika kuwaza huku na kuwazua… nikaanza kuvuta picha ya matukio ya siku tatu nyuma. Siku ya jumanne. Ambako nilifika maeneo ya Oysterbay, karibu kabisa na St. Peter's. Ghorofa jipya linaloitwa Jangid Plaza., floor namba 2, office namba 211 ambapo wanapatikana kampuni ya TMT.
Nakumbuka ilikuwa kama majira ya saa mbili hivi usiku. Nilikuwa hapa kusalimia na kupiga stori za hapa na pale. Wenyeji wangu, SirJeff (Ontario) na wenzake wawili raia wa Afrika Kusini, mmoja ambaye nilitambulishwa kama 'Mr . V' na mwingine 'Rea' niliwakuta wanajiandaa kufunga ofisi na kuondoka.

Ofisi ilikuwa ndio kama ina wiki moja tangu ifunguliwe, kwa hiyo nikatumia fursa hii kutalii na kuitazama uzuri wake na namna ambavyo ilikuwa imepangiliwa kwa ufasaha. Baada ya 'tour' ya kama dakika tano hivi, wote wanne tukaketi kwenye ofisi kuu ambayo walinieleza kwamba ndio ambayo inatumiwa na 'mentors'.

Baada ya kuketi kwa dakika kadhaa na stori za hapa na pale moyoni kuna jambo ambalo nilikuwa nataka kuwaeleza lakini moyo ukawa unasita. Kwa namna fulani sikuwa naona umuhimu wa kuwaeleza suala hilo lakini pia nilikuwa najiuliza kama kimaadili nitakiwa nafanya kitu sahihi kuwaeleza jambo hili.
Nikapima mawazo yangu kwa dakika kadhaa na baadae nikakata shauri.

Niseme kwamba binafsi namuona Ontario kama moja ya vijana muhimu zaidi kuwahi kutokea kwenye nchi yetu. Kwa kiwango ambacho tayari amesaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kutoa motivation pamoja na potential ambayo bado anayo kufanya kitu kikibwa zaidi.

Lakini zaidi ya hapo, kwangu binafsi ni mtu ambaye kila mara ambapo tukikutana lazima niondoke nikiwa motivated au tupeane new deals.
Kwa hiyo kitendo cha kuwa na taarifa ambayo inaweza kuwa na umuhimu kwake alafu nikakaa kimya tu nilihisi kama itakuwa ni namna fulani ya usaliti na nitakuwa sio 'mwana' kabisa.
Kwa hiyo nikavuta pumzi na kuamua kuwaeleza.

"You guys should put your sh*t together!" Nikawaeleza katikati ya mazungumzo.

"What do you mean!!" Yule jamaa ambaye nilitambulishwa kama 'Mr. V' akaniuliza kwa udadisi.

"Someone is asking questions about you guys!" Nikamjibu huku nikijitahidi kuongea 'casually'.

"Who?"

"Its not 'who'… you should be asking yourselves 'why'?" Nikamjibu. "Looks like someone wants you to shut down your oparetions here!"

Hawakushtuka sana kama ambavyo mtu mwingine angeshtuka. Baadae nikaelewa kwa nini hawakishtuka sana. Walikuwa na vibali vyote vya serikali kuwaruhusu kufanya biashara ambayo walikuwa wanaifanya. Kwa hiyo wazo la kwamba kuna mtu anaweza kuwafungia ofisi halikuwa realistic kwa kiasi fulani.

"Why wuold someone want to shut us down?" Yule jamaa akauliza tena.

"I dont know man… but 'someone' is asking questions! And its not good when 'someone' asks questions. I am just giving you guys the heads up… get you sh*t together!!"

Tukaendelea na maongezi kwa dakika nyingine kadhaa kisha wakafunga ofisi… wakanidrop somewhere na wao wakaelekea kupumzika.

Hiyo ilikuwa ni siku tatu zilizopita. Siku ya jumanne. Leo hii ijumaa mchana… watu wa vyombo vya usalama walikuwa wamefika kwenye ofisi za TMT pale Jangid Plaza, 'wakafunga ofisi', na kuwaweka staff wote chini ya ulinzi. Ndipo hapo ambapo nilipata taarifa hiyo na usiku huu nimefika hapa Kituo cha Oysterbay baada ya kusikia kwamba bado baadhi ya staff wa TMT wanashikiliwa.

"Aje chief..!"

Niligutuka kutoka kwenye kuwaza na kuwazua mfululizo wa matukio yaliyotokea baada ya kusikia nasalimiwa.
Nikaangalia alikuwa ni Ontario.

Tukasalimiana kisha akanieleza kinachoendeleo huko ndani. Kwamba kila kitu kiko sawa, inaonekana ilikuwa ni misunderstanding tu au watu hao wa usalama hawakuwa na taarifa sahihi kuhusu biashara ya Forex. Kikwazo kimoja tu ambacho kilikuwa kimebakia ni wale jamaa wa Afrika Kusini kupata vibali vya kazi nchini kwa sababu visa zao kwa madai ya watu wa Idara ya Kazi zilikuwa haziwaruhusu kufanya kazi. Kwa hiyo walikuwa wanatakiwa siku ya jumatatu kufika Idara ya kazi na kuanza utaratibu wa kupata nyaraka.

"So kila kitu kiko sawa?" Nikamuuliza.

"Everythibg is cool chief… thanks for the heads up za juzi… you werent kidding..!"

Tukacheka. Tukaagana. Nikaaondoka.

Kwa upande fulani moyo wangu ulikuwa na amani kwamba kwa upande wa TMT mambo yalikuwa yako sawia. Lakini upande mwingine nilikuwa nina hofu. Hofu ya kwamba dakika yoyote kuanzia sasa simu yangu itaita. Na kama simu ikiita lazima itakuwa ni simu ya 'bwana mkubwa' mmoja hivi.


Mpaka nafika nyumbani tayari ilikuwa karibia saa saba usiku. Kama ilivyo kawaida yangu ya kuandika hata paragraph moja tu kabla ya kulala, kwa hiyo nikaketi mbele ya kompyuta na kuanza kujaribu kuandika.
Lakini kadiri ambavyo nililuwa najitahidi kuandika, 'mzuka' wa kuandika ulikuwa hauji. Akili yangu na macho yalikuwa kwenye simu muda wote. Nilijua muda wowote ule itaita.

Ka karibia saa nzima nilijitahidi kutuliza akili niandike lakini wazo la simu kuita muda wowote lilikuwa limenitawala kichwani kiasi kwamba hakukuwa na uhalisia wa kuweza kuandika chochote usiku huu. Kwa hiyo ilivyofika saa nane kamili nikaamua kulala.

Sikujua kwa nini lakini siku ya leo nililala kupitiliza. Nilishtushwa na mlio wa simu asubuhi ya karibia saa tatu na nusu. Juu kwenye screen ilikuwa ni namba ambayo nilitarajia kuwa kuwa itapiga tangu jana.

"Shikamoo.!" Nikamsalimia.

"Bado umelala?" Akauliza swali bila kuitikia salamu.

"Yeah simu yako ndio imenishtua hapa!"

"Ofcourse you must be tired… sidhani hata kama umelala jana!"

Nikaanza kuelewa maongezi yanakoelekea.

"Ndio mzee!" Nikajaribu kuyapeleka maongezi mbele kwa haraka.

"Nasikia jana ulikuwa Oysterbay?" Akauliza kwa sauti ya 'kuinjoi'.

"Kuna shida?"

"Hapana… lets meet!"

Akanieleza kwamba tukutane ofisini kwake.
Niseme kwamba, huyu jamaa naamini ni moja ya watu wenye akili zaidi ambao nimewahi kukutana nao. Lakini pia ni moja ya watu wavivu zaidi ninao wafahamu. Kwa hiyo ilikuwa ni ajabu leo hii siku ya jumamosi kunambia kuwa tukutane ofisini.

Kama saa tano kamili hivi nilikuwa tayari nimefika ofisini kwake. Nilimkuta anaongea na jamaa anaitwa Robert (sio jina halisi) ambaye nafahamu anafanya kazi Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Nilipoingia tu wakamaliza maongezi yao na kuagana. Robert akaondoka na tukaanza kuongea na mimi. Tulipiga stori mbili tatu za 'warm up' mpaka tukafika kwenye maongezi yaliyonileta hapa.

"Ulikuwa unafanya nini Oysterbay jana?" Akaniuliza.

"He is a friend… and you guys were wrong… unajua jana…."

Kabla sijaendelea kubwabwaja akanikatisha kwa kuonua mkono.

"No no no… sijakuita kwa sababu hiyo!"

Nikamtumbulia macho tu.

"Nataka kufahamu kuhusu Forex!"

Nikamtumbulia macho zaidi. Nilihisi kama hakuwa serious hivi. Kwa sababu nilikiwa na hakika kabisa mpaka muda huu anafahamu forex ni nini.
Lakini aliendelea kuniangalia kwa uso wa kumaanisha kwamba alikuwa serious anataka nimueleze forex ni kitu gani.

"Ok Chief… kwa kadiri ninavyofahamu Forex Trading ni biashara ya currencies ambapo……"

Akanikatisha tena kwa kuinua mkono.

"Habib! Si umemkuta Robert hapa ametoka wakati wewe unaingia..?"

"Ndio!"

"Amenielezea yote hayo… global financial markets, currencies, kununua, kuuza…trading seasions, sijui pips, margins na mambo chungu mzima! Naelewa yote hayo… nataka wewe unieleze kile ambacho sikujui au pro kama Robert hawezi kukijua…"

Sasa nikamuelewa kwa nini alikuwa ameniita hapa. Bwana mkubwa huyu maongezi yetu mengi huwa yanahusu tafiti za masuala ya 'nyuma ya pazia'. Alikiwa anataka kufahamu kama najua chochote cha zaidi kuhusu biashara ya Forex ambacho "hakifundishwi darasani."


"Chief kuna mengi sana inaweza kutuchukua siku nzima!" Nikamwambia huku najiweka sawa kwenye kiti mkao wa fanani.

"Its suturday… i have the whole day"

"Ok sir!"

Nikaanza kutiririka.


NGUVU YA BIASHARA YA FOREX


THE BALCK WEDNSDAY

September 16, 1992

Jim Trott, Chief Dealer wa Benki Kuu ya Uingereza pamoja na timu yake walikuwa kijasho chembamba kinawatoka. Siku hii ya leo walikuwa wanaweka historia ya kununua Paundi kwa siku moja kwa kiasi ambacho kilikuwa hakijawahi kushuhudiwa na hakija shuhidiwa tena mpaka leo hii.
Lengo kuu lilikuwa ni kujaribu kuinua thamani ya Paundi dhidi ya fedha za kigeni hasa hasa Dola ya Marekani na Deutsche Mark ya Ujerumani (Kipindi hicho bado Ujerumani inatumia Deutche Mark).

Lakini kuna kitu kilikuwa hakiko sawa kwenye soko la dunia la fedha. Kadiri ambavyo walikuwa wananunua ilionekana kwamba kulikiwa na mtu, watu au kikundi cha watu walikuwa wanauza zaidi ya wao wanavyonunua.

(Tafadhali endelea kusoma nitaeleza hapo baadae kidogo hizi 'mechanism' za kuuza na kununua fedha zinavyofanyika na Benki kuu za nchi na Traders wakubwa)

Ikimbukwe kwamba katika katika kipindi hiki nchi ya Uingereza ilikuwa ni sehemu ya umoja wa ERM (Exchange Rate Mechanism) umoja ambao ulitangulia kabla ya kuanzishwa kwa European Union. Umoja huu dhima yake kuu ilikuwa ni kuhakikisha kwamba kila nchi ya Ulaya ilikuwa inaweka viwango 'fixed' vya Exchange Rate za sarafu zao badala ya kuachia soko liamue viwango hivyo.
Kuvunja kwa sharti hilo itakupasa kujitoa kwenye umoja wa ERM na kuwa kama kujipiga risasi ya kisiasa.

Katika kipindi hiki kutokana na uchumi wa Ujerumani kuwa imara kuliko chumi za nchi nyingine zote Ulaya hivyo 'exchange rate' za sarafu za kila nchi ilikuwa inatakiwa kuwekwa kurandana na thamani ya sarafu ya Ujerumani ambayo ilikuwa ni Deutsch Mark. Kwa mfano exchange Rate ya Paundi kwa Deutsch Mark (DM) ilitakiwa kuwa kati ya 2.78 mpaka 3.13.
(Nimeeleza kuwa nitaeleza kwa lugha nyepesi hizi mechanism)

Kitendo cha kuwa na kiwango kikubwa cha uuzwaji wa Paundi maana yake ni kwamba kulikuwa na jaribio la kuidondosha sarafu ya Uingereza. Lakini pia kitendo cha uuzwaji huu wa Paundi maana yake ni kwamba wauzaji hao walikuwa na hakika kuwa thamani ya Puandi itashuka. Kwa sababu kwenye biashara ya fedha ukiuza sarafu fulani ili upate faida inapaswa sarafu hiyo unayoiuza ishuke thamani. (Nitaeleza kama nilivyosema).
Kwa hiyo wauzaji hao walikuwa na hakika kwamba thamani ya Paundi itashuka. Hii ilikuwa haiingii akilini kabisa kwa kuwa kama ambavyo nimeeleza kwamba Uingereza ilikuwa ndani ya Umoja wa ERM na hawakuruhusiwa kushusha thamani ya Paundi chini ya exchange rate ya 2.78 dhidi ya DM. Na si hivyo tu Benki kuu ya Uingereza yenyewe walikuwa wanainunua Paundi.

Kwa hiyo kwa mantiki ya kawaida kabisa wafanyabiashara wa soko la fedha la kimataifa ili wapate faida kwenye Paundi walikuwa wanatakiwa kuinunua Paundi badala kuiuza. Lakini hali ilikuwa tofauti kabisa… kadiri muda ulivyokuwa unaenda kiasi kikubwa zaidi cha uuzwaji wa Paundi ulikuwa unafanyika. Ilimaanisha kwamba kuna mtu alikuwa anaona kitu ambacho wao wenyewe wenye Paundi yao, Benki Kuu ya England na serikali walikuwa hawakioni.

Kuna kitu hakikuwa sawa kabisa.

Waziri Mkuu wa Kipindi hicho John Major ikampasa kuitisha kikao cha dharura nyumbani kwake maeno ya Whitehall. Kikaoni walikuwepo wabunge wenye ushawishi kama vile Douglas Hurd, Kenneth Clarke, Norman Lamont pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Uingereza Mchumi Mark Carney. Wote walikuwa wanajaribu kukuna vichwa kujua ni nini ambacho kilikuwa kinatokea. Na ni kitu gani ambacho huyo anayeuza anakiona na wao hawakioni.

Japokuwa kikao hiki kilikiwa kinahusu masuala ya fedha lakini pia mmojawapo kikaoni alikuwa ni Bi. Dame Stella Rimington, Mkurugenzi wa shirika la Ujasusi la MI6 kipindi hicho.
Uwepo wake ulikiwa unatokana na mkanganyiko ambao ulikuwa unaendelea na Bi. Stella alikiwa na jibu moja tu la kuwasaidia labda.
Aliwaeleza kwamba hawezi kujua ni kwa nini hasa mtu huyo anaziuza Paundi kwa kiasi hicho kikubwa na kwa kasi (na amewezaje kuzimiliki kwa kiwangi kikubwa hivyo) kwa kuwa mtu huyo hata hayuko kwenye orodha hata ya watu elfu moja matajiri duniani. Pia hafahamu ni kitu gani ambacho mtu huyo alikuwa anakiona na wao walikuwa hawakioni. Lakinini wamefanikiwa kumtambua ni nani.

Aliwaeleza kwamba alikuwa ni Forex Trader mmoja tu, tena yuko nchini Marekani ambaye alikuwa amezua kitimu timu chote hicho ambacho wasipokuwa makini na kama mtu huyo yuko sahihi anaweza kuivunja Uingereza Vipande vipande na ikawabidi kumpigia magoti.
Lakini pia kilichokuwa kinashangaza zaidi ni kwa namna gani mtu mmoja aweze kuwa na uthubutu na ujasiri wa 'kubet' against uchumi wa nchi imara kama Uingereza? Kuna kitu gani alikuwa anakiona? Amepata wapi fedha zote hizo?? Kwa nini anaonekana ana uhakika na anachokifanya?

"Nataka kumjua ni nani?"

Waziri mkui wa Uingereza kilichokuwa kinamkereketa rohoni ni kumfahamu mtu huyo lakini shushushu mbobezi na Mkurugenzi wa MI6 Bi. Stella alikuwa anahisi wanapaswa kutafuta ufumbuzi wa nini hasa kilikiwa kinaendelwa bila wao kujua zaidi ya kufahamu ni nani huyo mtu.

"Hapana… nahitaji kumjua"

Waziri Mkuu wa Uingereza John Major akasisitiza kuwa anahitaji kumfahamu.

"Ok Sir… anaitwa GEORGE SOROS" Bi. Stella akamjibu.

Image result for george soros
George Soros


"Ni nani huyu mtu??"

Kwa hakika mpaka siku ya hii ya leo Septemba 16 mwaka 1992 hakukuwa na mtu yeyote muhimu duniani ambaye alikuwa anamjua George Soros. Lakini ndani ya masaa machache yajayo Ulimwengu mzima ilikuwa unaelekea kumfahamu George Soros. Binadamu pekee ambaye aliweza kuipigisha magoti nchi nzima ya Uingereza na kuiabisha serikali kwa tukio ambalo halitakuja kusahaulika mpaka siku dunia inafutika. Siku ambayo itakumbukwa daima. The Black Wednesday.



Inaendelea....

Imeandaliwa na The Bold | Jamii Forums

Post a Comment

0 Comments