Ni stori kutoka katika Mkoa mpya wa Songwe ambapo Mzee Ambilikile Panja mkazi wa Kijiji cha Majengo Kata ya Ihanda Wilaya ya Mbozi amefariki na kuzikwa akiwa na umri wa miaka 127.
Huyu Mzee amefariki katika Hospitali ya Vwawa wilayani Mbozi na inaelezwa kuwa ameacha mjane, watoto 24, wajukuu 113, vitukuu 282, vilembwe 157, vining’ina 25 na vilembwekezi wa 5.
Idadi ya watu katika familia yake ni 606 aliowaacha, sawa na idadi ya watu katika baadhi ya vijiji wilayani Mbozi.
Mzee huyu inasemekana kuwa ndiye binadamu mzee zaidi duniani na amevunja rekodi ya kumzidi mtu anayetambuliwa na Guinness Book of World Records Vailet Brown kwa miaka 10
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena