Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe, PC Zakayo Doto anadaiwa kumuua mwanajeshi wa JWTZ, Neema Masanja kikosi cha 514 KJ kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.Taarifa kutoka mkoani humo zinaeleza kuwa askari polisi huyo aliitelekeza Silaha aliyoitumia katika mauaji hayo na kutokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Pudensiana Protas amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo kwa kueleza kuwa chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana kwa sababu marehemu ameshafariki na mshtakiwa ametoroka.
Hata hivyo Afisa Mtendaji wa Kata ya Maguvani, Hafla Mbunju amesema kuwa chanzo kabisa kinachozungumzwa na watu wa eneo ambalo tukio limetokea ni wivu wa kimapenzi.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena