Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Tanzia | Mzee Kingunge Afariki Dunia

Taarifa zilizotufikia hapa RoryaFinest.com asubuhi hii ya leo ya February 2, 2018 ni kwamba Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo.
Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.
Mke wa Kingunge Peras Ngombalemwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi January kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo.
Katikati ya mwezi January mtoto wa marehemu, Kinjekitile aliiambia Ayo TV kuwa hali ya baba yake ilikuwa ikiendelea kuimarika kasoro miguu ambayo bado ilikuwa ikisumbua.

Post a Comment

0 Comments