Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | Saluti Za Kijeshi Maarufu Duniani (PICHA)

Related image
Wengi najua wanafaahamu kuwa salute ni alama tu inayotumika jeshini (duniani) kuonyesha heshima kwa aliyekuzidi cheo.Yah hiyo ndio maana yake halisi ila unapaswa kujua kuwa salute sio kwamba inatumika jeshini tu.
Taasisi mbalimbali duniani za watu binafsi hutumia salute kama salamu ya kila siku na hata JF tutaanza kusalimiana kwa salute na mimi ndio mwasisi wake(Sipo serious kwa hili).

Sasa leo sipo hapa JF kuongelea salute za kiraia isipo kuwa nipo hapa kuongelea salute za kijeshio zitumikazo duniani huko.

Kwanza kabisa kijeshi salute sio kazima ipigwe kwa kutumia mkono kama ambavyo mmekuwa mkiona kwenye movies nyingi za wazungu.Kuna njia nyingi za mwanajeshi kupiga salute.Mjeshi anaweza piga salute kwa kutumia mkono wa kulia au wa kushoto,pia anaweza asitumie mikono kabisa na still akafanikiwa kupiga salute hivyo hupaswi kulalili kuwa salute za kijeshi hupigwa kwa mikono tu.

[​IMG]

Salute za kijeshi zina mifumo yake,mfano salute za USA ni tofauti na zile za British Army au zile zinazotumika nchi za COMMON WEALTH .

Katika nchi ya UK ,salute anapigiwa mwanajeshi aliyepewa commission na malikia tu.Vivyo hivyo nchi zote za Commonwealth ni maafisa tu wa jeshi ndio wanaopigiwa salute.Naposema maafisa wa jeshi namaanisha wanajeshi wenye nyota kuanzia moja na kuendelea.



Salute inayopigwa British Army ndio hiyo hiyo inatumika na French Army.

Salute na USA ni tofauti na salute ya nchi za UK na France
[​IMG]
(Kushoto ni General wa USA alipokutana na General wa FRANCE,kulia)

Salutes zao ni tofauti kabisa.Nchi nyingi za Africa zinatumia salute ya kulia hapo juu

CHANZO CHA KUSALIMIANA KWA SALUTE

Salute inayotumika sasa ilianzia huko Ufaransa ambapo askari maofisa walipokuwa wakikutana walikuwa wanavua sehemu ya kofia zao ili macho yao yaonekane pale wanapopishana na wakubwa zao kijeshi.Hapa namaanisha kofia za askari wa France kipindi hicho zilikuwa hazina tofauti na Helmet ya bodaboda wa Kwetu UKONGA.

Ilikuwa ni ishara ya kujitambulisha kuwa "Mimi fulani na siogopi chochote"

USA Army wakaja na yao kama kuiendeleza ya ufaransa kwa kusema kuwa askari unapaswa kuvua kofia pale unapokutana na mwanajeshi aliyekuzidi cheo.Wanajeshi wakatii kwa kusalimia kwa kuvua kabisa kofia zao.

Mwaka 1745 Waingereza nao hawakuwa nyuma wakaja na yao wakisema mwanajeshi anapopishana na afisa wa jeshi asivue kabisa kofia bali anapaswa kuweka mkono wake juu ya kufia yake.Mfumo ukaendelea kufanya kazi.

Na hii ya Uingereza iliendelea kubadilishwa mpaka kuja hii tunayotumia saivi duniani.

SALUTE YA MKONO WA KUSHOTO:

[​IMG]

Baadhi ya wanajeshi wanaruhusiwa kusalute kwa kutumia mkono wa kushoto kama mkono wa kulia una majeraha yanayomzuia kusalue kwa mkono wa kulia(Case hizi ni mara chache sana )

Mwanajeshi ambaye atakuwa na siraha begani hasa bega la kulia ataruhusiwa kusalute kwa kutumia mkono wa kushoto ambao utakuwa free kwa wakati huo(Baadhi ya nchi).

SALUTE NDOGO:

[​IMG]

Mwanajeshi atakayekuwa amebeba 'sword' anaaina yake ya kusalute anapopita mbele ya mkubwa wake.Yeye atasalute tofauti kabisa na wenzake,ataiinamisha sword yake kuinamia chini na kugeuza sura yake walipo wakubwa wake anaowasalimia.Hii nayo ni salute!!

Salute za Hewani:

Hizi hutolewa na zile ndege za kijeshi zinazopita juu hasa wakati wa maonyesho ya kijeshi huko duniani.Ndege hii hupita sambamba na parade ikipita mbele ya wakubwa wa kazi nayo huunga kwa juu.Siku ya sherehe za uhuru nchi mbali mbali za Africa hufanya hii(Siku ya uhuru wa Kenya au Uganda nenda kaone )

[​IMG]


SASA TUONE SALUTE ZA CHACHE NYINGI DUNIANI:

Australia na New Zealand


Hawa kwa pamoja hutumia mfumo wa British Army ambapo mkono wa kulia hukunjwa nyuzi 45 na kiganjwa cha mkono wa kulia hunyooka huku mkono wa kushoto umenyooka kuelekea miguuni.

[​IMG]

Officers always saluted with the right hand (as the left, in theory, would always be required to hold the scabbard of their sword)[7] The salute is given to acknowledge the Queen's commission. A salute may not be given unless a soldier is wearing his regimental headdress,

British Army:

Kuanzia mwaka 1917 wanajeshi wa British Army walianza kusalute kwa kutumia mkono wa kulia ambapo kiganja hunyooka sana.Kiganga hicho hukaribia kugusa kofia.Ila kabla ya mwaka 1917,salute kwa wanajeshi ambao sio maafisa ,salute waliruhusiwa kupiga kwa mkono wowote ule ila maafisa ilikuwa ni kwa kutumia mkono wa kulia tu.

Kwa British Army,salute hupigiwa afisa wa jeshi tu na sio vinginevyo.Afisa wa jeshi ni wale waliopewa commission na Malkia tu na wana nyota kuanzia moja.

[​IMG]

CANADA ARMY:

[​IMG]

Askari wa Canada husalute kama waingereza,lengo likiwa ni lile lile kuonyesha heshima kwa aliyekuzidi cheo.

Sasa kwa hawa unatakiwa usimame wima ndio upige salute isipokuwa kama mwanajeshi alikuwa anatembea anatakiwa ageuze shingo uelekea alipo afisa kama ishara ya heshima na ndio salute yenyewe hiyo.

DENMARK ARMY:
Huko Denmark ni tofauti kidogo ambapo wao wana salute za aina mbili.Moja inatumiwa na jeshi la majini na angani na inafanana na ile inayotumika USA.
Ya pili ni ile inayotumika na wanajeshi wa ardhini.

Hii hufanywa kwa kunyoosha vidole vya mkono wa kulia na kuviinamishia chini vikiwa vimenyooka

[​IMG]

FRANCE ARMY:

Kwa hawa salute yao ni kama ya waingereza isipokuwa kwa kila salute inayotolewa hujibiwa kwa salute.

Nipigie salute nikupige salute pia.

Hawa salute haitolewi kama mwanajeshi atakuwa hajavaa sare zilizokamlika kuanzia kofia mpaka buti au kama mwanajeshi amebeba silaha hatoruhusiwa kusalute.


[​IMG]
(General wa France )

GERMAN ARMY :

[​IMG]

INDIAN ARMY:

India wanasalutes za aina tatu,Jeshi la ardhin,majina wanasalute kwa kutumia mfumo wa British Army
Kwa jeshi la ardhini husalute kwa kunyoosha kiganja mbele
upload_2018-3-9_14-39-41.png 

INDONESIA ARMY:

Huko ni kwenye salute sasa.Huko salute hutumika kuanzia mashuleni mpaka jeshini.Mtaani hawana habari za Good morning ,sijui shikamoo nop.Huko ni salute hadi gengeni na hata mkipishana chooni ni salute tu

[​IMG]

ISRAEL DEFENSE FORCES:

Huko salute sio salamu ya kila mda au kila siku.Salute ni heshima kubwa na hutolewa wakati wa sherehe za kijeshi tu.

[​IMG]


PAKISTAN ARMY:

Huko Pakistan,salute wanayotumia inafanana kabisa na ile inayotumiwa na British Army.Salute hutolewa kwa mkono wa kulia isipokuwa pale mkono wa kulia ukiwa na matatizo ndio hutumia wa kushoto .Vidole hunyooka kabisa na kugusa mwanzo wa kope za jicho lake la kulia.

Mwanajeshi mwenye cheo kidogo ndio humpigia salute mwenzie mwenye cheo kikubwa ila kama mwenye cheo kikubwa amevaa uniform full.

Pia kama mwanajeshi mwenye cheo kidogo ni dereva wakati huo na gari lipo kwenye motion hatoruhusiwa kupiga salute.

[​IMG]


SWISS ARMY:

Hawa ni wale wanajeshi wenye cheo kidogo wanatakiwa kuwasalute wenye vyeo vikubwa mda wowote wanapokutana.Mfano akiingia ndani tu unamsalute,akitoka tu una msalute.Akiinama una msalute na akiinuka unamsalute.

Wale mnaotaka kuwa wajeshi someni sana shule

[​IMG]

POLAND ARMY:

Huko Poland ,wanajeshi husalute kwa kutumia vidole viwili vya mkono wa kulia na hapo ni kwa waliovaa sare za jeshi kuanzia kofia mpaka kiatu.




[​IMG]


TURKEY ARMY:

Katika nchi ya Uturuki ,mwanajeshi anasuruhisiwa kutumia salute ya mkono kama kavaa kofia ya jeshi.
Kama atakuwa hajavaa kofia ya jeshi au ana silaha begani ataruhusiwa kuinua kichwa juu na kushusha kama ishara ya salute.


Anayepigiwa salute ni lazima arudishe salute

ALBANIA ARMY:

Hawa wanasalute ya kipekee duniani.Salute yao imetoka kwa muasisi wake jina Zog I

Salute hii hufanywa kw mkono wa kulia ambao huweka juu ya moyo huku kiganja kikiangalia chini.

Sheria za wapiga salute ni kama za British Army tu
[​IMG]


SANGWILE MAKAMANDA

Post a Comment

0 Comments