Miongoni mwa shutuma zilitoka katika kampuni ya ukusanyaji na Ukaguaji wa data za Trump kimtandao ambayo ilishtakiwa kwa kuiba data za watumiaji zaidi ya milioni 50.
Kutokana na tuhuma hizo hisa za Facebook zilipungua kwa 7% kufikia saa 7 usiku wa kuamkia Mach 20 na imekadiriwa kuwa zaidi ya dola billion 37 za thamani ya soko la hisa kwa siku husika zimepotea.
Upotevu huo wa fedha umemfanya Mark Zuckerberg ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook kushuka thamani kifedha kwa dola Billion 5.1.
Zuckerberg anamiliki 16% ya hisa za Facebook na sasa ana thamani ya dola 69.5 billion. Jarida la Forbes limeripoti kwa sasa Mark ameshuka hadi nafasi ya saba kwenye list ya matajiri duniani toka namba tano.
Facebook iliingia kwenye mtikisiko mwaka 2017 baada ya kutuhumiwa na Uingereza, Austria na Italia kwa kuchapisha habari zenye mrengo usiofaa kwenye mataifa hayo.
Zuckerberg, mwenye umri wa miaka 33, alianzisha Facebook mwaka 2004 akiwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19 katika chuo kikuu cha Harvard. Aliacha chuo ili apate kuzingatia muda mwingi kwenye kampuni hiyo. Kwa sasa Facebook ina watumiaji zaidi ya Billion 2 kila mwezi.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena