Dr. Robert Ouko alikuwa ni waziri wa mambo ya nje wa Kenya alipotea usiku wa tarehe 12 mwezi wa 2 mwaka 1990. Ouko alipotea akiwa katika shamba lake lililoko huko Koru karibu na Muhoroni. Tarehe 16, siku nne baada ya kupotea kwake serikali ilitoa taarifa kwamba mwili wake ulikuwa umepatikana katika kilima cha Got Alila karibu na yalipo makazi yake. Mwili wake ulikuwa umechabangwa mapanga kasha kuchomwa moto na ulikuwa umekutwa ukiwa na vitu mbalimbali ikiwemo bunduki, dumu la mafuta ya Diesel pamoja na kiberiti. Vyote isipokuwa hilo dumu la mafuta vilikuwa mali ya Ouko. Habari hii ya mauaji yake ilifanya mji wa Nairobi ulipuke kwa vurugu na maandamano.
Taarifa za mwanzo kutoka jeshi la polisi zilisema kuwa Ouko alikuwa kajiua, lakini haikuchukua muda kugundulika kwamba Ouko alikuwa ametesa, akapigwa risasi na mwili wake kuchomwa moto. Maswali na vurugu za wananchi zilimlazimu aliyekuwa raisi wa Kenya wakati huo Bwana Daniel Arap Moi kuomba makachero kutoka shirika la Uingereza lijulikanalo kama New Scotland Yard kusaidia katika upelelezi wa kifo chake.
Mwezi wa 10 mwaka 1990, Moi aliteua tume ya kusimamia uchunguzi juu ya tukio hilo ikiwa inasimamiwa na Mwanasheria anayejulikana kama Evans Gicheru ambaye baadaye alikuja kuteuliwa kama mwanasheria mkuu wa serikali. Kamati hii ilitenguliwa na kufutwa na Moi, mwezi wa 11 mwaka 1991, japokuwa haikuwahi kutoa ripoti yake ya mwisho lakini uchunguzi wake ulisaidia kuleta ukweli wa mambo mengi na kuufanya ujulikane kwa umma.
Baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo aliyekuwa waziri wa wa nishati, Bwana Nicholas Biwott na katibu wa wizara ya ulinzi wa ndani Hezekiah Oyugi, walikamatwa kwa ajili ya mahojiano lakini waliachiwa baada ya wiki mbili kutokana na ukosefu wa ushahidi juu yao.
Jonah Anguka, aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya, alishitakiwa kwa kupanga mauaji ya Ouku lakini alifutiwa mashitaka, hivyo kesi ilishindwa kutatuliwa. Baada ya hapo Anguko alitafuta hifadhi ya ukimbizi nchini Marekani kwa kuhofia maisha yake. Akiwa huko alitoa kitabu kinachojulikana kama “Absolute Power” akikana kuhsusika kwake kwenye mauaji ya Bwana Ouko. Wakati wa kesi juu ya Anguka ikiendelea, aliyekuwa mkuu wa wilaya wa Kisumu wakati Ouko alipopotea, Bwana Godfrey Matewakati Ouko alipopotea, aliieleza kamati kuwa ANguka aliingilia upelelezi wa kamati ya ulinzi baada ya mwili wa Robert Ouko kupatikana akiwa amekufa.
Uchunguzi uligundua kwamba Ouko alikuwa akiandaa ripoti kuhusu mwenendo wa rushwa kwenye serikali ya Kenya na jinsi rushwa ilivyo zuia mipango yake ya kufungua kiwanda cha kuzalisha Molasses katika jimbo lake. Ripoti hiyo haikuonekana baada ya mauaji yake na ilikisiwa kwamba mauaji hayo yalikuwa na lengo la kuzia hiyo ripoti isitoke.
Mwezi wa 3 mwaka 2003, serikali mpya ya Mwai Kibaki ilifungua upya uchunguzi wa kifo cha Ouko kwa kutengeneza kamati ya bunge ya kuchunguza suala hilo. Kamati hii ilipewa ushahidi kutoka kwenye uchunguzi wa makachero wa Uingereza kwenye uchunguzi wao wa mwaka 1990, ulio onyesha uhusika wa baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo Biwott, ambaye mpaka muda huo alikuwa akikana kuhusika na mauaji hayo, pia Oyugi ambaye kwa wakati huo alikuwa ni marehemu kwakuwa alifariki mwaka 1992. Mwezi wa 3 mwaka 2005, bunge liliamuru aliyekuwa raisi wa Kenya wakati mauaji yanatokea Bwana Arap Moi kuja bungeni kwa ajili ya kutoa ushahidi.
Kamati inaambiwa kuwa Moi ndiye aliyetoa amri ya kuawa kwa Ouko
Tarehe 4 mwezi wa 3 mwaka 2005, kamati ya bunge ya kuchunguza kifo cha Ouko, iliambiwa kuwa ni Raisi Moi aliyetoa amri ya kuawa aliyekuwa aziri wake wa mamvo ya ndani mwaka 1990.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Bwana Gor Sunguh alidai kuwa kachero wa Scotland Yard ajulikanaye kama John Troon, aliitaarifu kamati hiyo ilipomfuata London wiki mbili zilizopita, kuwa Dr. Ouko aliuwa kutokana na amri iliyotolewa kutoka kwenye mhimili mkuu. Bwana Sunguh alisema kuwa hii amri ya namna hii haitolewi na mtu mwingine bali raisi tu ambaye kwa wakati huo alikuwa Moi.
Aliendelea kudai kwamba kamati yake ilikuwa London wiki mbili zilizopita ili kuzungumza na Kachero John ambaye alipeleleza kwa kina kifo cha Ouko pamoja na kifo cha mshauri wa mambo ya biashara raia wa Uswiss Bi Marianne Brinner.
Sunguh aliendelea kusema kuwa, raisi alimfuta kazi Bwana Ouko ambaye alikuwa ni mbunge wa mji wa Kisumu wakati ule na kumlazimisha arudi kwenye makazi yake yaliyoko Koru, huku waliznzi wake wakiondolewa. “Hakuna mtu mwingine aliyekuwa na uwezo wa kutoa amri ya kuawa kwa Ouko” Sughuh alisema.
Sunguh aliendelea kudai kuwa kachero John alijaribu mara kadhaa kutaka kufanya mahojiano na aliyekuwa mbunge wa Keiyo Kusini Bwana Nicholas Biwott, kwakuwa ndiye aliyekuwa mshukiwa namba moja lakini mara zote alishindwa kwakuwa alikuwa akikingiwa kifua na Bwana Moi.
Barua kutoka British High Commission iliyoletwa mbele ya kamati ya Bwana Sughuh ilionyesha kuwa Troon alikuwa amekamilisha uchunguzi wake na aliitarifu serikali ya Uingereza kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha kumkamata na kumshitaki Bwana Biwott na viongozi wengine wa juu, ila Moi alikuwa amemzuia kwa kumnyima ruhusa ya kufanya hivyo.
Sughuh alidai kwamba kabla ya upelelezi, Moi alisema hakuna jiwe ambalo halitageuzwa katika upelelezi huo, lakini upelelezi ulipoanza mawe na vizuizi vyote viliwekwa kwenye njia ya wapelelezi. Aliendelea kudai kwamba uongozi wa Moi ulianzisha upelelezi wao uliofanyioka samababa na upelele wa John uliokuwa ukiendelea. Katika upelelezi uliofanywa na watu wa Moi Bwana Jonah Anguka aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kisumu wakati huo, alizuzishiwa makusudi kuwa ndiye mhusika wa mauaji ili uficha ukweli.
Pia maisha ya kachero John yalikuwa mashakani baada ya kuanza kupokea vitisho, hivyo ilimlazimu kuondoka nchini Kenya baada ya kupewa saa 72 za kuondoka. Sughuh aliongeza kuwa serikali ya Moi inahusika kwa kujaribu kuficha ukweli kwenye mauaji ya Bwana Ouko, na pia iliwaua mashuhuda wa mauaji hayo.
Sughuh alidai kuwa kamati yake imefanikiwa kupata angalau majina ya mashuhuda 100 ambao walikufa katka mazingira ya kutatanisha. Haya ni kati ya baadhi ya mambo ambayo inabidi yawe yalishajibiwa na Bwana Moi,inabidi tumsumbue, aliongeza Bwan Sughuh.
Inasikitisha sana kwamba kwa sasa tunaenda kumaliza uchunguzi wetu bila yeye kuhojiwa na kujibu ,aswali yetu. Japo kukataa uito wa kuitwa na bunge ni kosa kisheria lakini, lakini kamati haitochukua hatua zozote dhidi ya aliyekuwa raisi Bwana Moi.
Kwakuwa aliwahi kuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 40, makamo wwa raisi kwa miaka 13 na raisi kwa miaka 24, huyu bwana alipashwa kuwa muhamasishaji wa uongozi unaofuata sheria. Alisema Bwana Sughuh.
Moi asije kulalamikia kamati ikiwa itahitimisha kuwa alihusika katika baadhi ya mambo kwenye mauaji ya Bwana Ouko.
Mmojawapo wa wanakamati Bwana Kiema Kilonzo alisema kuwa kamati inamtaka Moi aeleze ni kitu gani kilitokea wakati alipotembelea Washington DC akiwa ameongozana na Bwana Ouko pamoja na Biwott, kwakuwa Ouko aliuawa wiki kadhaa baada ya wao kurudi kutoka katika safari hiyo.
Kilonzo alisema kuwa wangependa kusikia kutoka kwa MOi kama ni kweli alimpa Ouko likizo na kumlazimisha kurudi kwenye makazi yake yaliyopo Koru baada ya kurudi kutika Washington. Pia kamati ingependa kupata maelezo kutoka kwa Moi kuhusu picha iliyoletwa mbele yao na Bwana Biwott ikimuonyesha Moi akimpigia Ouko saluti kwa mkono wa kushoto.
Mwanakamati mwingine Bwana Raphael Wanjala alisema, “Ilikuwa ni muhimu sana kwetu kama raisi msataafu Bwana Moi kuwa hapa kwakuwa kazi ya kamati zote za upelelezi wakati wa utawala wake ziliharibiwa.”
Kamati ya Sunguh pia ilitaka Moi awambie kama yeye na Ouko walisafir kwa kutumia ndege moja wakatio wakitoka Washington .
Pia wailtaka maelezo juu ya ajali ya barabarni aliyopata Dr. Ouko tarehe 9, mwezi wa 2 mwaka 1990 wakati akielekea Kericho. Walitaka kujua kama iwapo pia raisi aliwasiliana na Ouko wakati akiwa likizo na kama alipokea nakala kutoka kwa Mkurugenzi wa makampuni ya BAK akilalamika kunyanyaswa na baadhi ya mawaziri.
Kachero John alikuwa pia kamtaja kama makamo raisi Hezekiah Oyugi, kama mmoja wa washuhukiwa wakuu wa mauaji ya Ouko. Oyugi alifariki kwa ugonjwa mwaka 1991.
Kamati wakati ikimalizia kutoa hotuba yake ya ripoti ya uchunguzi, mwenyekit wa kamati Bwana Sughuh alisema “Tuna taarifa kuwa genge la kiharifu lilipewa kazi ya kumuua Ouko na watu waliokataa kuhojiwa na kamati yetu. Genge hilo ilitakiwa lilipwe kshs 3,00,000, lakini baada ya genge hilo kudai kwamba pesa hiyo ni ndogo dau liliongezwa mpaka Kshs 8,000,000. Baadaye wanakikundi wa genge hilo la uhalifu waliua baadhi ya wenzao kwa kugombea pesa hiyo.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena