Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | IFANYE NYUMBA YAKO KUWA KIVUTIO KWA WATALII

IJUE NJIA MPYA YA KUFANYA BIASHARA YA UTALII TANZANIA, JE WAJUA NYUMBA YAKO NA MANDHARI YAKE NI KIVUTIO CHA UTALII NA KUWA SEHEMU YA KIPATO CHAKO?
Suala la utalii limekuwa ni nguzo kubwa ya uchumi katika nchi mbalimbali duniani na hii ni ukweli usiopingika kuwa utalii ndio umekuwa ukichangia zaidi katika ukuaji wa pato la taifa husika na hata kukua kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja. Makala hii leo inalenga kuwasaidia watanzania na wafanyabiashara wote wa kitanzania kupata njia mpya ya biashara ya utalii nchini ili kuyabadilisha maisha yao hususani katika ombwe hili la umasikini na ajira linaloikumba dunia kwa ujumla na ukizingatia Tanzania ni nchi pekee iliyojaaliwa kuwa na rasilimali nyingi na watanzania wanaweza kuzitumia ili kujipatia kipato kizuri. Je ni kwa vipi?

Watanzania mbalimbali tumekuwa tukijenga nyumba kubwa lakini tunaziacha hazina watu na wakati mwingine nyumba tunazoishi ni kubwa kuna nafasi zinabaki na nyumba hizo ziko katika maeneo mbalimbali yaliyo karibu na vivutio vya utalii kama vile karibu na hifadhi za taifa, mbuga za wanyama, viwanja vya ndege, mapango, na maeneo haya yako sehemu mbalimbali kama vile Dar es salaam, Kilwa, Tanga, Morogoro, Ngorongoro, Mikumi, Kilimanjaro, Manyara, Serengeti na maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii nchini.
Sehemu hizi ni muhimu sana na ndizo zinazoweza kukuza kipato chako na biashara yako kwani unachohitajika ni ubunifu tu wa kuboresha mazingira ya eneo lako utaweza kukaribisha wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi na ulimwenguni kote wanaofika kwaajili ya utalii na kuondoa ile dhana ya kufikia kwenye mahoteli makubwa tena yaliyo na bei ya ghali sana, na hivyo kukufanya wewe kupata wateja wengi wa kitalii kwa kutoa huduma ya malazi na kifungua kinywa kwa bei nafuu kabisa huku watalii wakifurahia utamaduni na huduma za makazi yako hapo ikiwemo lugha ya kiswahili.
Njia hii mpya ya kibiashara inaitwa “Malazi na Kifungua kinywa” ambapo njia hii imekuwa ikitumiwa na nchi mbalimbali duniani kama marekani, India, canada, Cuba, Indonesia na nchi nyingine nyingi na imeweza kuwasaidia wakazi mbalimbali wa nchi zao kunufaika na sio makampuni ya kigeni huku wakiita njia hii ni “Bed and Break fast”. Tanzania tunaweza kuthubutu maana ni njia ambayo inaingiza kipato kwa haraka. Hivi ni vidokezo ambavyo unaweza kutembelea kujionea jinsi biashara hii ilivyo maeneo mbalimbali duniani na uanze sasa.
Flipkey vacation homes and private rentals
www.flipkey.com
Tripadvisor holiday rentals
http://www.tripadvisor.com/Rentals
Roomorama - the alternative to Airbnb with most deals / coupons
https://www.roomorama.com/
Holiday Lettings - the UK alternative site to Airbnb
https://www.holidaylettings.co.uk/content/list_your_home
Wimdu - the European similar website to Airbnb
http://www.wimdu.co.uk/…
Only for travellers from Germany, the Netherlands, Switzerland
www.9flats.com
Hakika Tanzania tunaweza na sasa tuanze na makazi tuliyo yasahau kabisa.
Watanzania ni wakati wetu sasa kuufanya utalii utunufaishe sisi wenyewe wazawa wa nchi yetu na sio watu wengine na tujione sisi ni watu muhimi katika taifa letu, ilikuwa ni ndoto sasa inatimia tubadilishe maisha yetu sasa kwa kutumia nyumba zetu ambazo ni rasilimali zetu ili kuepukana na wimbi la umasikini na ninaamini kwa mtu mwenye kiu ya biashara na mtanzania mwenye kiu ya mafanikio atachukua hatua sasa kupitia makala hii.

Post a Comment

0 Comments