Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akimkabidhi Kadi ya CCM aliekuwa Kada na kiongozi wa Chadema Katika Mikoa ya Mwanza na Katavi. |
Aliekuwa Kada na Kiongozi katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema katika Mikoa wa Mwanza na Katavi Antony Charles Nongo, amekihama chama hicho na Kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.
Nongo alikuwa ni mwanachama wa Chadema tangu mwaka Elfu mbili na alifanikiwa kushika nyazifa mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho ambazo ni pamoja na Katibu Kata ya Buswelu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kabla ya kuhamia Mpanda Mkoani Katavi.
Akiwa Mpanda alikuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo pia alikuwa ni Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo uliopita wa Serikali za Mitaa kupitia Ukawa, huku pia akichaguliwa kuwa Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Mchangani Wilayani Mpanda baada ya Chama chake kutwaa Uongozi wa Kijiji hicho.
Akizungumza wiki iliyopita wakati akipokea kadi ya CCM, Nongo alisema kuwa amefikia maamuzi ya kutimka kutoka Chadema baada ya kubaini kwamba chama hicho kipo kwa ajili ya Maslahi, jambo ambalo linapelekea baadhi ya makada wake kutumika kwa ajili ya Maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa Chama hicho.
Alisema kuwa pamoja na kuitumikia Chadema Usiku na Mchana lakini amejikuta akikosa msaada kutoka ndani ya Chama hicho kutokana na kuuguliwa kwa muda mrefu na Mkewe ambapo ameongeza kuwa licha ya kuwa na mawasiliano mazuri na Viongozi wa Chama hicho bado hakupata ushirikiano wowote uliolenga kumsaidia mkewe kupata matibabu.
Nongo alikabidhiwa kadi ya Chama cha Mapinduzi wiki iliyopita katika Uwanja wa Msalaba Mwekundu Kisesa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu aliekuwa na ziara ya siku mbili Wilayani Magu ambapo pia Wanachama wapya 23 wa Kike waliweza kujiunga na CCM Wilayani Magu na kukabidhiwa kadi za uanachama.
MSIKILIZE HAPA CHINI ANTONY CHARLESAntony Charles Nongo akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi wa CCM wiki iliyopita katika Uwanja wa Msaba Mwekundu Kisesa Magu. |
Wasichana waliokabidhiwa kadi za Chama cha Mapinduzi CCM wakila kiapo cha uaminifu kwa ajili ya kukitumikia chama hicho. |
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwasili katika Uwanja wa Msalaba mwekundu Kisesa Wilayani Magu ambapo pia Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya ya wazazi wa CCM Kiwilaya yalifanyikia. |
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akihutubia katika Uwanja wa Msalaba Mwekundu Kisesa Wilayani Magu yalipofanyikia Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya ya wazazi wa CCM Kiwilaya yalifanyikia. |
Wananchi wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu (Hayuko pichani) katika Viwanja Msalaba Mwekundu Kisesa Wilayani Magu. |
Wachezaji wa Mpira wa Pete kutoka Timu Kisesa wakijiandaa kwa ajili ya Mchezo wao wa Kirafiki na Timu ya Bujora. |
Wachezaji wa Mpira wa Pete kutoka Timu Bujora wakijiandaa kwa ajili ya Mchezo wao wa Kirafiki na Timu ya Kisesa. |
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatuturu akisalimiana akisalimiana na Timu ya Watoto Kisesa. |
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwa tayari kuzindua mchezo wa Mpira wa pete baina ya Timu ya Kisesa na Bujora. |
Hapa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatuturu alikosa gori |
Hapa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatuturu akielekeza mpira langoni. |
Hapa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatuturu akizamisha mpira. |
Miraji Mtaturu akionyesha uwezo wake. |
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akijiandaa kupiga Mpira kama ishara ya uzinduzi wa mechi kati ya Kisesa na Bujora iliyochezwa katika Uwanja wa Msalaba Mwekundu Kisesa Wilayani Magu. |
Goooooooooooo.................Hatimae Miraji Mtaturu akazamisha Mpira wavuni. |
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena