Bamia ni mboga ambayo inafahamika na watu wengi na imekuwa
ikitumiwa na watu wengi hapa nchini Tanzania.
Pamoja na bamia kuwa mboga, lakini pia inafaida nyingi
katika miili yetu, licha ya kuwa wengi wetu huwa hatufahamu faida zake zaidi ya
kula tu kama mboga.
Miongoni mwa faida za mboga hii ni
pamoja na kusaidia kuondosha vimelea vya sumu kwenye ngozi, inasaidia pia
kuimarisha afya ya nywele na kuongeza kinga ya mwili.
Pia bamia husaidia kuondoa uchovu wa
mwili na msongo wa mawazo pamoja na kusaidia kutibu tatizo la kukosa choo.
Aidha, bamia pia inaelezwa kusaidia
kusafisha damu, kutibu mafua, vidonda vya tumbo, inaimarisha mifupa pamoja na
kuwa kinga ya magonjwa kama utapiamlo na anemia.
Mbali na hayo bamia pia inasaidia kutibu magonjwa
mbalimbali ya zinaa
kama vile kaswende na kisonono. Vilevile inaponya
tatizo la kwenda
hedhi mara kwa
mara na chango la kike.
Hizo ni baadhi ya faida za ulaji wa
bamia, endapo utaendelea kutembelea tovuti hii mara kwa mara basi utazidi
kupata elimu zaidi juu ya namna vyakula mbalimbali na mimea vinavyoweza kuwa
tiba nzuri na kinga ya magonjwa.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena