Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MICHEZO | BLATTER NA MSIMAMO WAKE NDANI YA FIFA

BLAAA
Wakati uchaguzi mkuu wa Shirikisho al soka duniani FIFA ukitarajiwa kufanyika kesho mjini Zurich Uswiss, Rais anayewania nafasi hiyo kwa mara nyingine Sepp Blatter amekataa kujiuzulu nafasi hiyo.
Blatter ameshinikizwa kujiuzulu baada ya shirikisho hilo kukumbwa na kashfa ya rushwa ambapo tayari Maafisa saba kutoka FIFA wakishikiliwa kutokana na tuhuma za rushwa
.
Rais wa Shirikisho la soka Ulaya, Michael Platini amesema Blatter amekataa wito huo wa kujiuzulu na uchaguzi wa FIFA utafanyika kama ulivyopangwa.
Platini amesema UEFA itashiriki uchaguzi huo kesho na imewashauri washirika wake kumpigia kura mpinzani wa Blatter aliyebakia Ali-Hussein kutoka Jordan.
Afrika pamoja an Asia wameahidi kumpigia Blatter kura.

Post a Comment

0 Comments