Header Ads Widget

Responsive Advertisement

HABARI | UZEMBE WA MUUGUZI WAIGHARIMU HOSPITALI

Masuala ya uzazi wa mpango ni moja ya mambo ambayo yamekuwa yakihimizwa sana katika nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania pia.

Sasa leo kuna hii stori kutoka kwa majirani zetu hapo Kenya ambapo Mahakama nchini humo imeiamuru hospitali moja maarufu kulipa faini ya dola zaidi ya elfu 48 kwa kushindwa kuzuia uzazi.

Adhabu hiyo inafuatiwa baada ya Jaji kubaini kuwa mmoja wa wahudumu wa hospitali ya Agha Khan alizembea katika kupachika mwilini dawa ya kuzuia utungwaji wa mimba iliyochaguliwa na mwanamke kwenye mkono wake, licha ya kwamba mwanamke huyo alifanyiwa upasuaji mdogo kwa ajili ya kuzuia uzazi.

Aidha, taarifa zinasema kuwa muathirika aliimbia mahakama hiyo kuwa yeye na mumewe walikuwa tayari na watoto wawili na kwamba hawakutaka kupata mtoto mwingine . Kwa hiyo kutokana na ushauri wa hospitali mama huyo alipachikiwa dawa ya kuzuia uzazi ambayo ingelimzuia kupata ujauzito kwa miaka mitatu. Lakini mwaka mmoja baadae aligundua kuwa alikuwa mjamzito.

Muathirika wa tukio hilo aliendelea kuieleza mahakama kwamba mimba ambayo hakuipanga ilimsababishia maumivu na mfadhaiko mkubwa , msongo wa mawazo, matatizo ya kifedha na matatizo ya unyumba.

Hata hivyo, Jaji alisema kuwa mshitakiwa ambae ni Hospitali ya Aga Khan , iliwasilisha nyaraka , lakini haikuwepo mahakamani wakati wa kesi hiyo.

Pamoja na hayo, kesi iliendelea na hatimae jaji aliamua kuwa mhudumu wa hospitali alizembea kazini . Aliamuru mama aliyeshitaki hospitali ya Aga Khan alipwe fidia ya dola elfu tano kwa hasara iliyosababishwa na apewe malipo ya dola elfu 43,000 za gharama ya maisha mtoto tangu kuzaliwa hadi atakapotimiza miaka 18

Post a Comment

0 Comments